MKE WA RAIS WA ZIMBABWE KUSHTAKIWA NA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU KUTOKANA NA KUFANYA UJANJA KATIKA ELIMU.
Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Zimbabwe al maarufu Zinasu, umesema kwamba unawasilisha kesi mahakamani hii leo kutafuta ufafanuzi zaidi wa namna mkewe rais Grace Mugabe alivyopata shahada ya udaktari wa falsafa.
Mwanafunzi mmoja mwanaharakati amesema kuwa ni muhimu kwa taifa hilo kuhifadhi hadhi yake ya elimu.
Baadhi ya watu wamehoji kasi aliyosomea shahada hiyo huku wengine wakidai ni njama za kumuandaa kwa urithi wa kiti cha rais baada ya rais Mugabe.
Gazeti moja linalomilikiwa na serikali , the Herald limechapisha kuwa Bi Grace Mugabe alipata shahada hiyo kwa utafiti wake juu ya mabadiliko ya mfumo wa kijamii na miundo ya familia.BBC
0 comments:
Post a Comment