BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE TANZANIA (TAMWA) NAMNA ILIVYOWANOA WAPIGA PICHA KURIPOTI MATUKIO YA UKATILI NA UNYANYSAJI WA KIJINSI DAR ES SALAAM.

Mkufunzi mafunzo ya upigaji Picha, Mwanzo Millinga akitoa maelekezo kwa wapigapicha Juma Mtanda (katikati) Rashid Mkwinda kulia na Erinest Kibandawa kushoto wakati wa mafunzo ya upigaji picha za unyanyasaji wa kijinsia na ukatili na maisha ya mwanamke yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kuhusisha wapigapicha wa vyombo habari kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar yaliyofanyika kwa siku mbili Novemba 25 na 26 jijini Dar es Salaam.
Wapiga picha Rashid Mkwinda kushoto, Juma Mtanda na Halima Kambi wakiangalina picha katika kamera wakati wa mafunzo ya upigaji picha za unyanyasaji wa kijinsia na ukatili na maisha ya mwanamke yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (TAMWA).

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika ofisi za Tamwa jijini Dar es Salaam.

Hapa Mkufunzi, Mwanzo Millinga akifundisha namna yautendaji kazi wa kamera na namna ya kutumia vipimo ili kuweza kupata picha iliyobora.

Mpiga Picha Mkuu wa The Guardian Ltd Seleman Mpochi naye akitoa mafunzo katika mafunzo hayo, Kutoka kushoto ni Mustafa Kapalata na Bertha Mjema.

Huyu anaitwa Fredrick Katunda mhariri wa kanda gazeti la Mtanzania akielekeza jambo kwenye mafunzo hayo.

Mwandishi kutoka Zanzabar Mwinyimvua Abdi Nzukwi akichangia mada huku Humphrey Shao akitafakari jambo katika mafunzo hayo.

Joachim Mushi kulia akifutilia jambo na mwenzake.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari Wanawake (TAMWA), Valerie Nsoka wa tano kutoka kulia waliosimama mstari wa pili na Mkufunzi wa mafunzo ya upigaji picha, Mwanzo Miliinga wa kwanza mstari huo kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wapigapicha wa vyombo mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya upigaji picha za kijinsia na maisha ya mwanamke kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar yaliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania (Tamwa) jijini Dar es Salaam. wa nne kutoka kulia waliochuchumaa ni mpigapicha mkuu wa The Gurdian Ltd, Seleman Mpochi.Chanzo/ Mtanda Blog.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: