FREEMAN MBOWE, MAALIF SEIF SI LOLOTE SI CHOCHOTE MBELE YA CCM, CCM YAWAONYESHA JEURI UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2014.
Freeman Mbowe.
MATOKEO ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika mwishoni mwa wiki kote nchini, yameendelea kuanikwa na kuonesha CCM imeendelea kung’ara.
Lakini, pia CCM imevuruga ngome muhimu za viongozi wa kambi ya upinzani, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Ukawa, Freeman Mbowe wilayani Hai mkoani Kilimanjaro na Mwenyekiti wa CUF na Kiongozi mwenza wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba wilayani Tabora.
Aidha, imeiteketeza ngome ya Katibu Mwenezi wa NCCR-Mageuzi, David Kafulila, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini mkoani Kigoma katika tarafa ya Nguruka.
CCM yang’ara kwa Mbowe Licha ya Wilaya ya Hai kutajwa ndilo shina na ngome ya Chadema, bado CCM imeendelea kuibuka na ushindi mnono katika ngazi ya vijiji na vitongoji.
Msimamizi wa uchaguzi, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Hai, Melckzedek Humbe, alisema wilaya hiyo yenye vijiji 62 , CCM imeshinda vijiji 37 na Chadema vijiji 23.
Kijiji cha Sanya Station jana kilitarajiwa kufanya uchaguzi na kijiji cha Kwa Sadala, kikisubiri baada ya mgombea wa CCM kufariki dunia.
Alisema katika vitongoji 295, CCM imeshinda vitongoji 163 na Chadema Vitongoji 126 huku Chama cha Wananchi (CUF) kikipata kitongoji kimoja, huku vitongoji 5 vikifanya uchaguzi wake jana.
Alisema katika nafasi za Viti Maalumu CCM imepata 310, Chadema 171, ambapo katika wajumbe wa halmashauri ya vijiji mchanganyiko, CCM imepata 416 Chadema 282.
Akifafanua matokeo hayo, Humbe alisema kata ya Machame Mashariki yenye vijiji 5, CCM imeshinda vijiji vyote vitano na vitongoji 18, na Chadema haikupata kijiji lakini kilipata vitongoji 4.
Kata ya Rundugai CCM imeshinda Vijiji 5 na vitongoji 17, na Chadema vijiji 2 na vitongoji saba. Alisema Kata ya Weruweru yenye vijiji 4 na vitongoji 17, CCM imeshinda vijiji vyote 4 na vitongoji 14, huku Chadema ikikosa vijiji na kupata vitongoji vitatu.
Katika kata ya KIA, CCM imeshinda vijiji 2 vitongoji 12, Chadema ikipata vitongoji viwili, huku kijiji kimoja cha Sanya Station matokeo yakiwa bado. Humbe alisema kata ya Narumu yenye vijiji 4 na vitongoji 16, CCM imeshinda vijiji 3 na vitongoji 12, Chadema ikipata kijiji kimoja na vitongoji 4, ambapo kata ya Uroki CCM ilipata vijiji 2 na vitongoji 6, huku chadema ikipata vijiji 2 na vitongoji 10.
Katika kata ya Machame Mashariki yenye vijiji 5 na vitongoji 16, CCM imeshinda vijiji 4 vitongoji 11, Chadema ikipata kijiji kimoja na vitongoji 5, ambapo kata ya Romu CCM imeshinda vijiji 3 na vitongoji 12, huku Chadema ikipata vijiji 2 na vitongoji 6.
Humbe alisema alisema kata ya Masama Kusini, Chadema imeshinda vijiji 2 vitongoji 9, na CCM ikipata kijiji kimoja na vitongoji 7, ambapo kata ya Masama Magharibi Chadema imeshinda vijiji 3 na vitongoji 8, huku CCM ikipata vijiji 2 na vitongoji 8.
Kata ya Masama Kati yenye vijiji 5 na vitongoji 18, Chadema imeshinda vijiji 4 vitongoji 13, CCM imeshinda kijiji kimoja na vitongoji 5, ambapo Kata ya Machame Kaskazini CCM imeshinda kijiji kimoja na vitongoji 10, ambapo Chadema ikishinda vijiji 4 na vitongoji 19.
Humbe alisema katika kata ya Mnadani, CCM imeshinda vijiji 3 vitongoji20 huku Chadema ikishinda vijiji 3 na vitongoji 18, huku kata ya Machame Magharibi Chadema imeshinda vijiji vyote viwili na vitongoji 9 na CCM ikishinda vitongoji vitatu.
Katika mamlaka ya mji mdogo wa Boma Ng’ombe, Kata ya Bondeni yenye vitongoji sita, CCM imeshinda vitongoji vyote, ambapo kata ya Muungano yenye vitongoji 6 Chadema imeshinda vitongoji vyote.
Kata ya Boma yenye vitongoji 5, CCM imeshinda vitongoji 2 na Chadema vitongoji 3. Msimamizi wa uchaguzi, ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rombo, Mohamed Maje alisema katika vijiji 68 vya wilaya hiyo, CCM imeshinda vijiji 34 vitongoji 147 na Chadema vijiji 22 na vitongoji 80, ambapo vitongoji 70 uchaguzi wake utafanyika Jumapili ya Desemba 21 kutokana na kasoro mbalimbali zilizojitokeza.
Hali tete kwao Profesa Lipumba Lucas Raphael kutoka Tabora anaripoti kuwa katika wilaya ya Uyui, anakotoka Profesa Ibrahim Lipumba, CCM imefanikiwa kushinda katika vijiji 130 na vyama vya upinzani vijiji 26 kati vijiji 156. Kwa upande wa Vitongoji, CCM imeshinda Vitongoji 589 katika wilaya hiyo na vyama vya upinzani vitongoji 108, kati ya Vitongoji 697.
Kwa upande wa Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Manispaa hiyo yenye vitongoji 159, CCM imeshinda vitongoji 121 sawa na asilimia 93, Chadema wamepata vitongoji 5 sawa na asilimia 3 na CUF wamepata vitongoji 4 sawa na asilimia 3.
Kafulila apata pigo Fadhili Abdallah aliyepo Kigoma anasema Kafulila amepata pigo baada ya kushindwa kufanya vizuri katika uchaguzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Uvinza, Nicholous Kombe alisema tarafa ya Nguruka yenye vijiji 19, NCCR imefanikiwa kupata kiti kimoja na CCM imenyakua jumla ya viti 16 huku uchaguzi katika vijiji viwili umeahirishwa na sasa utarudiwa.
Matokeo hayo yanaonesha kuwa nyumbani alikozaliwa Kafulila katika mji mdogo wa Uvinza, Kata ya Uvinza yenye vijiji vitatu, CCM imenyakua nafasi zote za wenyeviti wa vijiji huku kikinyakua viti 12 vya wenyeviti wa vitongoji na ushirikiano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakichukua viti vitano.HABARILEO
0 comments:
Post a Comment