Mfanyakazi wa nyumbani aliyenaswa kwenye kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani leo.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa anajutia kile alichokifanya na hata kuomba msamaha. Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.
Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la ,mauaji, kiongozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.
Bi Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.
Kesi hio imeakhirishwa hadi Jumatano, wakati ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.
Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola 800 au adhabu zote mbili.BBC
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kimataifa
/ HOUSE GARL ALIYEMTIMBANGA MTOTO KWA KUMKANYAGA AOMBA MSAHAMA UGANDA, KUKUMBWA NA ADHABU YA KUTOZWA FAINI YA DOLA 800 KAMA ADHABU.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment