BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBRAZIL EMERSON WA YANGA OUT.

http://www.mwanaspoti.co.tz/image/view/-/2537904/highRes/886198/-/maxw/600/-/2o3r1q/-/emerson.jpg
Taarifa za usajili na kuachwa wachezaji zinazidi kuingia na safari hii inasemekana kuwa kiungo Mbrazil Emerson amekuwa mhanga wa kwanza wa kuondoka kwa kocha Mbrazil Marcio Maximo baada ya mchezaji huyo kuachwa na Yanga.

Mbrazil huyo anaondoka Yanga baada ya kucheza mechi moja pekee dhidi ya Simba ambako Yanga ilifungwa 2-0.

Emerson alishindwa kuwaridhisha mashabiki wa Yanga ambao wengi walionyesha kukerwa na uwezo mdogo wa kiungo huyo katika dakika 45 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Simba.


Moja ya vichwa vya habari vilivyokuwa vimepambwa na habari kumhusu Emerson.

Emerson alikuja nchini siku chache zilizopita ambapo alipaswa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji Genilson Santos Santana Jaja ambaye hakurudi baada ya kuondoka nchini kufuatia kusimama kwa ligi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: