BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

POLISI MORO SC YAWASHIKA MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA YANGA, SAID BAHANUZI NA BEKI WA ZAMANI WA KCB YA KENYA, MESHACK ABEL MOROGORO.

Mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro SC, Issa Bushir kulia akimwelekeza jambo mlinzi mpya wa klabu hiyo Meshack Abei huku akishudiwa na Afisa Habari, Clement Bazi kushoto na mjumbe Mokili Lambo wakati wa kusaini mkataba wa miezi sita ya kuitumikia klabu ya polisi Moro katika ofisi kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro.


Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mlinzi kisiki wa zamani wa klabu za KCB ya Kenya, mtanzania Meshack Abeil amesaini mkataba wa miezi sita na Polisi Moro SC ikiwa siku moja tu baada ya maafande hao kuinasa saini ya mshambuliaji, Said Bahanuzi tayari kutumikia katika mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2014/2015.



Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi mjini hapa, mara baada ya kumalizana na klabu ya Polisi Moro SC, Abel alisema kuwa amesaini mkataba wa miezi sita na amejiandaa vyema kukabiliana na changamoto za ligi kuu Tanzania bara na baada ya kumalizika kwa mkataba wake ataangalia kama anaweza kuendelea kukipiga na maafande hao.



Abel ambaye amewahi kutumikia klabu za Mtibwa Sugar, Simba na taifa star alisema kuwa wapenzi wa klabu ya Polisi Moro SC na wadau wa soka mkoa wa Morogoro watarajie mambo mazuri katika mzunguko wa pili.



“Nimesaini mkataba wa miezi sita na klabu ya Polisi Moro SC na kitu kinachoomba ni ushirikiano na wachezaji wenzangu.”Alisema Abel.

Said Bahanuzi mshambuliaji mpya wa klabu ya Polisi Moro SC.
 
Naye mshambuliaji mpya wa Polisi Moro SC, Said Bahanuzi aliyejiunga kwa mkopo akitokea klabu ya Yanga SC alisema kuwa kitu anachoomba ni ushirikiano na wachezaji wenzake ili aweze kutekeleza majukumu yake ya kupachika mabao.



“Unajua kitu cha msingi kwangu hapa Polisi Moro SC kwanza ninachoomba ni ushirikiano nzuri na wachezaji wenzangu ndani na nje ya uwanja lakini hata na wapenzi, uongozi na wadau wa soka sambamba na uzima ili kutuitendea haki klabu.”Alisema Bahanuzi.



Bahanuzi alisema kuwa ana imani kubwa klabu yake hiyo mpya itakuwa moto wa kuotea mbali katika mzunguko wa pili kutokana na kuona wachezaji waliosheheni vipaji sanjari na usajili nzuri uliofanywa na benchi la ufundi katika dirisha ndogo.



“Nitashirikiana na wenzangu kuhakikisha Polisi Moro SC inapata matokeo katika michezo ya mzunguko wa pili ligi kuu Tanzania bara.”Alisema Bahanuzi.



Mwenyekiti wa klabu ya Polisi Moro SC, Issa Bushiri alisema kuwa lengo la klabu ni kujaza nafasi zote tano za kusajili wachezaji katika dirisha ndogo kama kanuzi za TFF zinavyorhusu.



Bushiri alisema kuwa mpaka sasa tayari wamewasaainisha wachezaji wanne akiwemo Iman Mapunda (huru), Zohor Pazi (Simba SC), Said Bahanuzi (Yanga SC) na Meshack Abel (KCB Kenya) na kama watapata mchezaji mzuri kabla ya kufunga dirisha la usajili waatamsajili kiungo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: