BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA ULANGA NAMNA ILIVYOWACHOMEA MOTO NYUMBA NA MABOMA WAFUGAJI WAKATI WA OPERESHENI YA KUWAONDOA KINGUVU MOROGORO.

Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Igata kijiji cha Mbalinyi kata ya Biro tarafa ya Ngohelanga wakiishi katika mazingira magumu eneo la Nakasisi baada ya nyumba na maboma yao zaidi ya kaya 120 kuteketezwa kwa kuchomwa na moto kufuatia wafugaji kudaiwa kuishi katika hifadhi ya msitu wa kijiji hicho wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, tukio hilo lilitokea mwishino mwa mwezi wa 10 mwaka huu baada ya serikali ya wilaya ya Ulanga kuendesha operesheni hivi karibuni. Picha Juma Mtanda.
 Na Juma Mtanda, Morogoro.
Wafugaji katika wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro wanakabiliwa na changamoto lukuki huku baadhi yao wakiendelea kukumbwa na misukosuko kadha wa kadha na adha mbalimbali zinazotokana pengine na wao kushindwa kufuata taratibu ama sheria ziliwekwa na vijijini vinavyounda wilaya hiyo.



Kijiji cha Mbalinyi kilichopo kata ya Biro tarafa ya Ngohelanga wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro ni moja ya vijiji vyenye wafugaji wengi na kupelekea baadhi yao kudaiwa kuvunja sheria na kujikuta wakivamia ardhi iliyotengwa kwa matumizi mengine na kugeuza sehemu ya malisho jambo lililowakasirisha watawala ngazi ya wilaya.


Kutokana na hali hiyo serikali ya wilaya hiyo ya Ulanga Oktoba 29 hadi 31 mwaka huu iliendesha operesheni ya kuwaondoa wafugaji kwa nguvu kwa madai ya kuvamia hifadhi ya msitu na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo za kilimo, ufugaji na malisho sambamba na kugeuza makazi ya kudumu ndani ya msitu wa Igata na kusambaratisha miti kupungua kwa kiasi kikubwa jangwa likipiga hodi.


Changamoto nyingine wanazokumbana nazo wafugaji hao ni kushindwa kufuata taratibu hasa za mpango wa matumizi bora ya ardhi na kujikuta wakitumbukia katika adhabu ambazo pengine wangeweza kuziepuka bila kuleta madhara kwao kutoka kwa serikali kwani adhabu hizo zimekuwa zikiwarudisha nyumba kimaendeleo kwa kupungua kwa mifugo yao au kupigwa faini kubwa na kujikuta watu wa kuhamahama pasipo na makazi maalum kwa kukwepa utekelezaji wa maamuzi dhidi yao yanapotokea wameenda kinyume na miongozo ndani ya vijiji.


Wilaya ya Ulanga ni mojawapo ya wilaya za Tanzania ambayo zinafuata mpango wa matumizi bora ya ardhi, lengo likiwa kuepusha migogoro baina ya wakulima na wafugaji ambao wamekuwa na muingiliano mikubwa na wakati mungine kuzuka kwa vurugu na kupelekea mapigano yanayosababisha watu kupoteza maisha.


Mpango wa matumizi bora ya ardhi katika wilaya ya Ulanga kwa baadhi ya vijiji umekuwa sio wa kuridhisha kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kusimamia vyema na kusababisha msuguano baina ya wakulima, wafugaji na serikali, na serikali inapoona viongozi wa vijiji wameshindwa kutekeleza majukumu yao huingilia kati na muathirika mkubwa huwa mfugaji tofauti na mungine wa ardhi.


Darubini ya serikali ya Ulanga inamulika msitu wa Igata na kubaini uwepo wa wafugaji walioingia kimakosa na uhalibifu wa mazingira, sasa inaanza mchakato wa kutoa notisi ya miezi sita ya kuwataka wafugaji kuondoka kwa hiyari lakini wafugaji wana puuzia notisi hiyo nini kinafuata ?.


Masanja Msafiri (47) mkazi wa kijiji cha Mbalinyi anaelezea namna wafugaji walivyoondolewa ndani ya hifadhi ya msitu Igata na adha wanazopata baada ya serikali kuwaondoa kwa nguvu na mchakato mzima namna ulivyoendeshwa wa kuwatimua.


Msafiri anasema kuwa zoezi la kuwaondoa wafugaji katika msitu wa Igata kwa nguvu lilifanyika kwa siku tatu, ambapo oktoba 29, oktoba 30 na oktoba 31 mwaka huu ndiyo askari polisi ikishirikiana na mgambo wa kata za Biro, Ngohelanga na wale wa kijiji cha Mbalinyi walifanya operesheni kwanza ya kukamata mifugo katika mazizi nyakati za usiku majira ya saa 9 hadi saa 10 alfajiri kisha kuwasomba na kuwapeleka katika uwanja wa shule ya msingi kijijini hapo.


Katika siku tatu hizo za operesheni, novemba 01/na 02/ 2014, askari polisi, mgambo na maafisa wengine wa ngazi ya kijiji na wilaya baada ya kuhakikisha kazi ya kuondoa mifugo yote na mali za wafugaji hao kuona imemalizika, operesheni ilihitimishwa kwa kumalizia uchomaji moto nyumba na maboma ambapo yalibakia na kuhakikisha hakuna wafugaji wote eneo hilo.


“Hii opereshni imesababisha upotevu wa mali kama baadhi ya wafugaji kupotelewa na kiasi kikubwa cha fedha, kuku na nguo, chakula na vyombo vya ndani kwani wakati wanaamusha wafugaji na kuamuru kutoa mali zilizopo ndani baadhi zilikuwa zinasalia ndani ya nyumba ama boma kutokana na nyakati zenyewe zikichangia na usahalifu.”alisema mfugaji huyo.


MAMA AELEZA ADHA YA OPERESHENI.
Wande Shabaan (27) yeye alielezea tukio hilo kwa kusema kuwa, familia yake yenye zaidi ya watu 20 wanaishi katika mazingira magumu eneo la Nakasisi kwa kulala nje chini ya mti huku watoto wakilala katika kibanda kilizofunikwa mifuko ya nailoni.


Wakati wafugaji wakilalamikia kusanyanyasika katika operesheni hiyo, hifadhi ya msitu wa Igata ulitengwa rasmi mwaka 2014 na uongozi wa serikali ya kijiji cha Mbalinyi eneo la Igata kama sehemu ya kunufaika na faida mbalimbali misitu, uongozi wa kijiji cha Mbalinyi inaeleza namna wafugaji walivyovamia msiti na kuharibu mazingira.


Kaimu afisa mtendaji wa kijiji cha Mbalinyi kata ya Biro wilaya ya Ukanga mkoa wa Morogoro, Petro Msaliboko alisema kuwa eneo la Igata ulitengwa na kijiji mwaka 2004 ili kuwa hifadhi ya msitu kabla ya kuvamiwa na makundi ya wafugaji kuanzia mwaka 2006 kabla ya operesheni ilipofanikiwa kuondoa novemba 02 mwaka huu 2014.

Msaliboko alisema kuwa chanzo cha kuvamiwa kwa hifadhi ya msitu wa Igata ulianza kuvamiwa mwaka 2006 mmoja wa wafugaji aliyeuziwa eneo jirani na hifadhi hiyo na mwananchi wa kijiji cha Mbalinyi lakini kadri siku zilivyoenda yule mfugaji alianza kuwakaribisha wafugaji wenzake mwaka 2008 na 2009.


Viongozi wa serikali ya kijiji cha Mbalinyi mwaka 2009 iliona hali hiyo na kutafuta mbinu ya kuwaondoa wafugaji lakini ilizidiwa nguvu na mwaka 2010 ilibainisha kwa kuwekaa alama za mipaka na mwaka 2012 ilirejea tena kufanya operesheni ambayo nayo ilishindikana kuwaondoa pia.


“Wafugaji walimiminika na kujazana katika hifadhi ya msitu wa Igata na baadaye yaligeuzwa makazi rasmi ikiwemo kufanya shughuli za kilimo na ufugaji hali iliyopelekea msitu huo kuharibiwa kutokana na shughuli za kibinadamu.”alisema Msaliboko.


Hifadhi ya msitu wa Igata ina ukubwa wa heka 978, lakini aisa mtendaji huyo wa kijiji cha Mbalinyi anamshukuru Rais Kikwete kwa kuwaamrisha wakuu wa mikoa kujenga majengo ya maabara ya sayansi kwa kila shule za sekondari za kata kwani kwao imesaidia mkuu wa wilaya yao, Francis Miti kufika kijiji kwao kuhamasisha wananchi kujitolea katika nguvu kazi na wananchi kupata nafasi ya kutoa kero nyingine ikiwe ya uvamizi wa msitu wa Igata.


“Tunashukuru amri ya JK ya kuwataka wakuu wa mikoa kusimamia ujenzi wa majengo ya maabara ya shule za sekondari za kata kwani hali hiyo imesaidia mkuu wa wilaya yetu kutoa amri ya kumtaka kila mwananchi kuweka nguvu zake lakini wananchi walimpachika swali kwa nini amesimamia kidede katika ujenzi wa majengo ya maabara huku msitu wa Igata ukiendelea kutekea na wafugaji aliulizwa swali mkutanoni.”alisema Msaliboko.


Swali hilo lilisaidia, mkuu wa wilaya kuona ipo haja ya kutoa askari na viongozi wengine kutekeleza maombi yao ya kufanikisha operesheni ya kuwaondoa wafugaji ili mambo yaende sawa.

Februari 11 mwaka huu ilitolewa notisi ya miezi sita ya kuwataka wafugaji kuhama kwa hiyari na baadhi yao walitii amri hiyo na kuondoka katika hifadhi ya msitu wa Igata lakini wengine walikaidi notisi hiyo.


Msaliboko alisema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wafugaji kutoka mwaka 2012 kwani awali kijiji ilisajili wafugaji 58 na mifugo 1258 lakini idadi ya wafugaji iliongezeka na kufikia 106 na kuwa na mifugo 2480 kwa mwaka 2014 na ongezeko ambalo linapingana na mpango wa matumizi bora ya ardhi.


“Hawa wafugaji ni watu ambao sio wakweli kwani baada ya serikali kuona idadi yao inaongezeka siku, mwezi hadi mwaka, uongozi wa serikali ya kijiji iliona hali hiyo na kufanya maamuzi ya kuwapokea walioongezeka na kuwataka wahame Igata na kuhamia maeneo ya Ngakwela, Lungula, Kiyolwa, Makutano ambapo maeneo hayo walipewa na serikali yetu lakini waliuzia wenzao na wenyewe kurudi Igata wasikotakiwa.”alisema Msaliboko.


Halmashauri ya wilaya ya Ulanga mwaka 2010 ilitoa zaidi ya mizinga 30 kwa vikundi mbalimbali vya ufugaji nyuki katika kijiji cha Mbalinyi na kutegwa katika msitu wa Igata lakini matokea yake mradi huo haukuwa na maisha kutokana na mizinga hiyo kuondolewa juu ya miti na wenzao wa jamii ya wafugaji waliovamia msitu huo.alisema Msaliboko.


Novemba 07 mwaka huu mwandishi wa makala haya alifika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ulanga mkoa wa Morogoro, Francis Miti ili kupata ufafanuzi juu ya operesheni ya kuwaondoa wafugaji wanaodaiwa kuvamia hifadhi ya msitu wa Igata na mikakati ya serikali juu ya matumizi bora ya ardhi ambapo hakufanikiwa kuonana kutokana na kuwa safarini...........Itaendelea tena kesho. 
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: