BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SERIKALI YA ULANGA NAMNA ILIVYOWACHOMEA MOTO NYUMBA NA MABOMA WAFUGAJI WAKATI WA OPERESHENI YA KUWAONDOA KINGUVU MOROGORO.

Wakazi wa kitongoji cha Igata kijiji cha Mbalinyi kata ya Biro tarafa ya Ngohelanga wakiangalia mabaki ya nyumba na maboma yaliyoteketezwa kwa kuchomwa na moto kufuatia kuondolewa kinguvu na serikali, wafugaji wanadaiwa kuvamia na kuishi katika msitu wa hifadhi wa kijiji hicho na kusababisha zaidi ya kaya 120 kuishi katika mazingira magumu ikiwemo chini ya miti eneo la Nakasisi wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro, tukio hilo lilitokea mwishino mwa mwezi wa 10 mwaka huu. Picha Juma Mtanda.

Toleo iliyopita tuliona namna wafugaji walivyoondolewa kwa kuchomewa nyumba moto lakini hapa uongozi unatolea ufafanuzi, tuendelee katika sehemu ya pili na mwisho....

Ilifanya jitihada za dhati na kuonana na katibu tawala wilaya ya Ulanga, Steven Mapunda ambaye naye ilimlazimu kuwaita watalaamu wa idara za misitu, kilimo, mwanasheria mkuu wa halmashauri, afisa wanyamapori ili waweze kutoa maelezo kulingana na namna serikali ya Ulanga inavyoendesha mambo mbalimbali ikiwemo usimamizi wa sheria na taratibu zinazoongoza hasa katika sekta ya mifugo, kilimo na misitu.


Afisa misitu wilaya ya Ulanga mkoa wa Morogoro, Tumaini NnkoElisha yeye anaeleza katika kikao hicho kilichoitishwa na katibu tawala wilaya ya Ulanga hiyo kwa kusema kuwa operesheni ya kuwaondoa wafugaji iliendeshwa katika misingi ya haki na amani bila shuruti na zoezi lilifanyika nyakati za majira ya 12 asubuhi na kufikia kikomo majira ya saa 12 jioni.


NnkoElisha anasema kuwa kabla ya uchomaji nyumba na maboma moto walizingatia haki ikiwa safu mzima ya serikali ikiwa na jukumu la kusimamia ambapo kazi kubwa ya uhamishaji wa mali ndani ya nyumba ama katika boma kwa kuondolewa vitu vyote, zoezi la uchomaji moto lilifanywa na wafugaji mwenyewe kisha kuteketeza kwa kuchoma moto.


“Kilichofanyika kwa askari, mgambo na maafisa wengine ni kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa hasa kusimamia kikamilifu utoaji wa mali zote ndani ya nyumba ama boma na baada ya hapo mfugaji mwenyewe alihusika kuchukua jukumu la kuteketeza kwa kuchoma moto boma au nyumba lakini kazi hiyo ilifanyika baada ya kusaini kitabu chetu kama amekubaliana na mpango wa operesheni yetu kwani operesheni ni halali.”alisema NnkoElisha.



Meneja utawala bora na haki za binadamu shirika la juiya ya mashirika ya wafugaji na warina asali (Pingos Forum).


Naye Meneja utawala bora na haki za binadamu shirika la juiya ya mashirika ya wafugaji na warina asali (Pingos Forum) Emmanuel Saringe anasema kuwa Serikali imekuwa ikikumbwa na malalamiko mengi kutoka kwa wafugaji kutokana na kupitisha amri zinazowakandamizi wafugaji bila kufuata taratibu za ukamataji wa mifugo wakati wa utekelezaji wa operesheni.

Serikali inapotekeleza operesheni za kuwaondoa wafugaji maeneo yanayodaiwa kuvamiwa na wafugaji katika ardhi za vijiji, inaweza kuwa inafanya kazi hiyo kihalali lakini inashindwa sehemu ya kumwelekeza wapi wafugaji hao waende, haielezei nini hatima ya wananchi hao ambao ni wakazi halali wa vijiji hivi ikiwa wanakosora ya uvamizi wa maeneo tu ?.



“Kuna vitendo vinatokea vya uchomaji nyumba moto au maboma ya wafugaji na wanapowaondoa watu kwa nguvu bila kueleza wapi wakaishi na kufanyia shughuli zao za ufugaji huo ni unyanyasi na kukihuka haki za wafugaji hao.”alisema Saringe.


Saringe anasema kuwa kuna matatizo mengi ndani ya serikali za vijiji kwa kurudia rudia kufanya makosa yanayopelekea wafugaji mbeleni kuathirika kutokana na serikali za wilaya kushindwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara ya kuwakumbusha majukumu yao ikiwemo suala la utoaji wa ardhi kwani limekuwa na changamoto na kuzalisha migogoro siyo kwa wafugaji bali kwa wawekezaji.


“Serikali za vijiji na wilaya wanakosea, mfano ulio hai kijiji cha Mbalinyi wamewaacha wafugaji kwa kuishi ndani ya msitu wa Igata uliotengwa mwaka 2004 na kupita miaka 10 ipite alafu ione wafugaji walivamia na wanaosimamia sheria na taratibu wanaangalia bila kuchukua hatua katika kipindi hicho ?alihoji Saringe.


Aliongeza kwa kusema kuwa badala yake serikali imetumia nguvu kubwa na kujitokeza kwa adha na ukiukaji wa haki za binadamu kwa kulazimika kuwahamisha wafugaji katika msitu wa Igata kwa kuchoma moto maboma na kuwaacha wafugaji wakihangaika lakini wakati wakiomba kuingia katika kijiji viongozi huwalaghai wananchi hao wafugaji kwa kuchukua michango yao ya maendeleo kana kwamba wanaishi kihalali bila ya kuwataarifu uhalali wao wa kuishi kinyume na sheria.


Meneja huyo wa utawala bora na haki za binadamu shirika la juiya ya mashirika ya wafugaji na warina asali (Pingos Forum) alitoa wito kwa serikali kuwa ingekuwa vyema kama serikali kabla ya kuazimia kuwaondoa wafugaji kwa operesheni kubwa kuandaa maeneo ya kuelekeza maeneo ya malisho badala kuaacha wafugaji wakitapatapa kwani wanachanchi hao wanachangia maendeleo ya taifa.


Saringe alisema kuwa serikali itambue kuwa wafugaji wanapohamahama mara kwa mara imekuwa ikiwarudisha nyuma kimaendeeleo ya watoto wa wafugaji upande wa elimu kutoka na kuhama hama kunakotokana na kumbia eneo moja kwenda lingine chanzo kikiwa operesheni lakini ifikie wakati serikali imuone mfugaji kama raia wa Tanzania.

Aliongeza kwa kusema kuwa kusambaa kwa mfugaji maeneo mbalimbali ya Tanzania sio kwa kupenda bali ni katika kuangalia eneo lenye malisho ambapo utulivu wa mfugaji eneo moja utachangia watoto wao kupata eleimu bora ndani ya vijiji vilivyokaribu na malisho na endapo linakosekana hilo wanajikuta wakiishi maisha duni.


Lakini kwa upande wa Afisa tawala wilaya hiyo, Steven Mapunda katika kikao hicho kilichojumuisha waandishi wa habari yeye alitoa wito kwa mashirika mbalimbali ya kutetea haki za wafugaji nchini kusaidia kutoa elimu ya utambuzi wa sheria lakini na kueleza kuwa wafugaji wenyeji sasa inawapasa kufikia wakati waone misitu ina tija kubwa kwa maisha ya binadamu na si kwa mfugaji tu.


Mapunda alieleza kuwa katika kikao hicho kuwa kuna wakati kuna kasoro zinafanywa na baadhi ya viongozi ngazi ya serikali ya vijiji katika hasa katika suala zima la mchakato wa uombaji ardhi kwa matumizi mbalimbali na kwenda kinyumbe na taratibu na sheria na ugawaji.



Mapenda alisema kuwa kijiji kina uwezo wa kugawa ardhi kwa hekta 50 lakini baada ya kupitia taratibu zote, kinachojitokeza kwa wale viongozi wa serikali za vijiji wanaposhindwa kufuata taratizo hizo hugawa ardhi hekta 100 pengine na kuendelea jambo ambalo linaendana kinyume na taratibu na siku ya siku hulete migogoro.


Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini baadhi ya viongozi wa vijiji kuwa wamekuwa wakitumia mwanya wa uelewa mdogo wa wafugaji na kupokea fedha za wafugaji wakati wa uombaji ardhi kwa ajili ya malisho na kuwaelekeza kwenda popote napotaka bila kuwaelekeza na mfugaji kujikuta anakwenda katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya hifadhi ama matumizi mengine.



Lakini baada ya muda kwa wafugaji kukaa ndani ya kijiji husika na kujitokeza kwa kero zinazochangia mifugo kuingia katika mashamba ya wakulima pengine kwa bahati mbaya ama makusudi, serikali ya ngazi ya wilaya huendesha operesheni ambayo wafugaji ndiyo muathirika mkubwa na kuacha upande wa viongozi wa kijiji ukikenua meno hivyo serikali hiyo ya wilaya sasa ione haja ya kuwaadhibu na viongozi hao kama sehemu ya fundisho.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: