Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi kata ya Sabasaba, Mudhihil Shoo wa tatu kutoka kushoto akiwaongoza wanachama na viongozi mbalimbal wa chama hicho katika maandamano yaliyoanzia ofisi za kata hiyo hadi kweenye uwanja wa mtaa wa Konga kwa ajili ya kufanya kampeni ya mwisho ya uchaguzi wa serikali za mitaa katika Manispaa ya Morogoro.
Na Juma Mtanda, Morogoro.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood amewaomba wananchi wa Manispaa ya Morogoro kuwachague wenyeviti wa mitaa watakaowalea maendeleo hasa wanaogombea kupitia chama tawala cha mapinduzi (CCM).
Abood alitoa wito huo Mjini hapa wakati akizungumza katika kampeni za kuwanadi wagombea wa CCM katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ya Manispaa ya Morogoro.
Alisema kuwa wananchi wanapaswa kuwa makini kwa kuwachagua viongozi watakawaondolea kero mbalimbali zinazowakabili hasa kuangalia mgombea wa CCM.
Katibu Mwenezi wa CCM wa Wilaya ya Morogoro, Maulid Chambilila, alisema mitaa mingi inakabiliwa na kero nyingi zinazohitaji viongozi bora kuzishughulikia lakini nawaomba wananchi wawachague wagombea wa CCM.
WILAYA YA KILOSA:
Baadhi ya wananchi katika mitaa kadhaa ya Kata za Mkwatani na Mbuni, wilayani Kilosa, wamewekewa pingamizi ili wasipige kura katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa madai kuwa si wakazi wa maeneo hayo.
Habari zilisema pingamizi dhidi ya wananchi hao wanaodaiwa kuwa ni mamluki, zimewekwa na wenao wanaojiita kuwa ni wazawa wa kata hizo.
Hata hivyo wasimamizi wa uchaguzi katika maeneo hayo walikuwa wanaendelea kushughulikia pingamizi.
KATA YA MJIPYA MANISPAA YA MOROGORO.
Katika Kata ya Mjipya, mjini Morogoro, Ofisa Mtendaji Paul Ndelwa ametupilia mbali pingamizi nane zilizowekwa na CCM dhidi ya wagombea wa CUF na Chadema.
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake, Ndelwa alisema kwa upande wa CUF wagombea waliokuwa wamewekewa pingamizi ni Shabaan Hussein anayegombea katika Mtaa wa Fumilwa C na Said Hussein anawania uenyekiti katika Mtaa wa Simu A.
Ndelwa alitaja wagombea wa Chadema ambao pingamizi dhidi yao zimetupwa kuwa ni, Omari Mvambo, anayegombea katika Mtaa wa Fumilwa B, Gasper Dege wa Fumilwa A na Jamila Mbegu wa Mtaa wa Mbegu.
Wengine ni Sharifa Mnola wa Mtaa wa Ngoma A,Mussa Jumanne na Salum Mwandule wa Mitaa ya Makabuli A na B.
0 comments:
Post a Comment