BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AJALI ILIYOUA WATU 50 ENEO LA CHANGALAWE IRINGA ILIPANGWA NA BINADAMU, SERIKALI YATUPIWA LAWAMA.

 

Basi la Majinja likiwa limeangukiwa na kontena na kusababisha vifo katika eneo la Changalawe mafinga, hivi karibuni.

Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuendelea kwa ajali za barabarani. Picha na Venance Nestory


Dar es salaam.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi taifa ,James Mbatia amesema kwamba ajali iliyotokea eneo la Mafinga Changalawe mkoani Iringa ilikuwa imepangwa na binadamu na wala sio mipango ya Mungu.



Akizungumza jijini leo Mbatia amesema ajali hiyo ilipangwa na watendaji wa serikali kwa sababu ajali hiyo ilisababishwa na shimo kubwa ambalo limekaa kwa muda mrefu eneo hilo pasipo juhudi zozote za Serikali kulikarabati.


Mbatia amesema hawezi kukaa kimya ni lazima awasilishe suala hili bungeni ili wahusika wachukuliwe hatua kwa kuacha shimo kubwa barabarani kwa muda mrefu bila kuliziba.


Amesema shimo hilo ambalo ndio hasa lilikuwa chanzo cha ajali hiyo ni la muda mrefu lakini viongozi wa serikali wanaliangalia tu bila kuchukua hatua ya kuliziba.


‘’Jamani watanzania waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo ni wengi na ni aibu kwa taifa, ukizingatia chanzo cha ajali hiyo ni shimo la muda mrefu ambalo linaangaliwa na viongozi wetu kila siku bila kuliziba’’alisema Mbatia


Amesema ajali hudokeza kwa ujumla matokeo mabaya ambayo labda yangeweza kuepukwa au kukingwa ikiwa matukio yaliyosababisha ajali hiyo yangetambuliwa na kurekebishwa kabla ya tukio.


Amesema madereva wanaoendesha magari ya abiria wanatakiwa kupelekwa shule angalau kwa miezi sita ikiwa ni pamoja na kupimwa afya mara kwa mara.


Aidha ameitaka serikali kutoa tamko kuhusu ajali hiyo na sio kukaa kimya mpaka waanze kupigiwa makelele na wananchi kupitia vyombo vya habari.


Watu zaidi ya 40 waliokuwa kwenye basi la kampuni ya Majinjah Express lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam, walifariki papo hapo katika ajali hiyo iliyotokea jana wengine 23 wakijeruhiwa.MWANAMKE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: