Rashidi Mvungi baba wa Marehemu Nasra Mvungi ameondolewa katika shtaka la mauaji baada ya upande wa ushahidi kutomtia hatiani na hivyo shitaka kubaki kwa washatakiwa wawili.
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro imeondoa shitaka hilo kwa Mvungi baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa dhidi yake kuwa hana hatia.
Shitaka la mauaji kwa sasa limebaki kwa Mariam Saidi ambaye ni mama mkubwa wa Nasra Mvungi na Omary Mtonga mume wa Mariam Saidi ambao walikuwa wakiishi na mtoto Nasra kwa kumfungia katika boksi kwa muda miaka mitatu.
Mtuhumiwa Omari Mtonga akiwa chini ya ulinzi baada ya kugoma kutoka kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi wakati wakati akirudishwa katika chumba cha mahabasu mara baada ya kusikiliza kesi inamkabiri ya mauaji ambapo kesi hiyo sasa itasikilizwa katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam. Picha Juma Mtanda.
Mwendesha mashtaka wa serikali mkaguzi msaidizi wa polisi Aminatha Mazengo akisoma shitaka la mauaji mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya hiyo Irvan Msacky,kwa washitakiwa hao wawili alidai mahakamani hapo kuwa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.
Mazengo alidai kuwa kesi hiyo kwa sasa tayari imefunguliwa katika mahakama kuu wa kanda ya Dar es salaam na kwamba inasubiri vikao vya mahakama kuu ili iweze kusikilizwa.
Akitoa maelezo ya kuondolewa kwa Rashidi Mvungi katika kesi hiyo Hakimu mkazi Irvan Msacky alisema kuwa ameondolewa katika shitaka la mauaji kutokana na ushahidi kutoteshereza na kutomtia hatiani moja kwa moja na hivyo kuondolewa katika kesi ya mauaji.
Wakati kesi hiyo ikiwa imemalizika kusikilizwa,mshtakiwa Omary Mtonga alianzisha zogo kwa kutaka apatiwe mwendeno wa kesi ya awali kabla ya kupelekwa ngazi ya mahakama kuu kanda ya Dar es salaamu.
Aidha kutokana na kuonyesha hali hilo mwendesha mashataka Mazengo alimweleza Mtonga kuwa hiyo ni haki yake ya msingi kupatiwa mwenendo wa kesi yake hivyo atapatiwa hati hiyo kabla ya kurudishwa magereza,kuwa ilikuwa katika hatua ya uchapishaji.
Hata hivyo Mtonga baada ya kujibiwa hivyo hakuridhika na kuendelea kugoma kutoka ndani ya mahakama hali iliyomlazimi hakimu mkazi Msacky kuwaamuru askari kumuondoa kwa nguvu mahakamani hao ili iweze kusikiliza kesi nyingine.
0 comments:
Post a Comment