MBEYA CITY YAITIBULIA SIMBA SC MICHUANO YA KIMATAIFA AFRIKA.
Siku ya mwisho kabisa Simba kukanyaga uwanjani kucheza mechi za kimataifa ilikuwa Machi 3,2013 huku ikilala mabao 4-0 pale Angola kwa Recreativo Libolo na kuaga mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kipigo cha mabao 5-0 kwani ikiwa Dar es Salaam kabla, ilikula bao 1-0.
Baada ya Azam kutetereka kwenye mechi mbili zilizopita, Simba imeanza mchakato mgumu na wenye malengo maalumu kuhakikisha hata sekunde moja haipotei kuanzia katika mchezo.
Lakini jana Jumamosi Simba SC ilidondokea pua kwa Mbeya City kwa kutandikwa bao 2-0.
Nyodo za mashabiki wa Yanga SC ambazo zimekuwa zikitolewa na kuwatambia kutokana na ufiti wake wa hivi karibuni pamoja na ufanisi wake kwenye Ligi ya ndani na michuano ya kimataifa.
Simba ilianza kula sahani moja na Azam ambao ilikuwa ikiwaombea mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kupoteza mechi wao dhidi ya Kagera Sugar lakini Azam ikaibuka na ushindi waa bao 2-1 huku yenyewe Simba ikicharazwa bakora 2-0 na kuwafanya ndoto yao ya kutua nafasi ya pili wakiikodolea macho usiku na mchana bila mafanikio.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na vita kali ya nafasi ya pili kati ya Azam na Simba ambapo kocha mkuu wa Simba, Goran Kopunovic, alieza kuwa kikosi chake kinatakiwa kuhakikisha kinapata pointi tatu jijini Mbeya lakini halikuwezekana hilo na kuiombea mabaya Azam iteleza tu wajikite katika nafasi hiyo ya pili na kupanda ndege kwenda kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Lakini Mbeya City wametibua kila kitu katika mchezo wao uliopigwa Sokoine Mbeya kwani kwa mchezo huo Mbeya City walihitaji ushindi ili wajinasue na hatari ya kushuka daraja.
Katika maandalizi ya mchezo huo Kopunovic aliwafanyisha wachezaji wake mazoezi ya dakika 95 mpaka 100 wiki iliyopita ili kuwajengea uwezo wa kupambana na wababe hao wa Jiji la Mbeya ambao wanaonekana kuwa na pumzi ya kuhimili vishindo vya dakika 90 bila kuchoka.
Beki wa Simba, Joseph Owino alisema: “Hizi ni mechi za mwishoni na hakuna mechi rahisi kwa sasa, kila mmoja amejipanga kushinda, ila naamini tutafanya vizuri, City ni wazuri na mechi ya kwanza walitufunga hivyo tutahakikisha mechi hii tunapata ushindi.”
Lakini badala yake wakaambulia kipigo cha bao 2-0.
Katika mchezo wa Mbeya City, Simba ilimkosa mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi mwenye kadi tatu za njano na beki Hassan Kessy aliyeondolewa kikosini wakati Mbeya City iliwakosa straika Themi Felix anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu na kiungo Steven Mazanda ambaye ni majeruhi.
Kutokana na rekodi baina ya klabu ya Simba SC na Mbeya City, Mbeya Cty ndiyo imeonekana kuwa wababe kwa Simba SC baada ya kuikung'a Simba michezo miwili huku Simba ikiambulia sare mbili katika michezo minne walizokutana wababe hao.
0 comments:
Post a Comment