VITA YAHAMIA NAFASI YA PILI KWA KLABU YA SIMBA SC KUTAKA KUIPIGA KIKUMBO AZAM FC KATIKA MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA.
Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wameendelea kuuhakikishia umma wa mashabiki wake kuwa bado wanasaka nafasi ya pili kwa udi na uvumba baada ya kutoa kipigo cha bao 3-0 dhidi ya Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara, katika mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo.
Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba Jonas Mkunde alipachika bao dakika ya nane baada ya kuachia shuti kali nje ya eneo la hatari baada ya walinzi wa Ndanda kufanya makosa na mpira kujaa wavuni moja kwa moja.
Lakini haikuishia hapo, Simba waliongeza goli la tatu katika dakika ya 15 kupitia kwa Ramdhan Singano 'Messi' kutokana na uzembe uliofanywa na mlinda mlango wa Ndanda baada ya kuutokea mpira na kuukosa.
Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi dhidi ya wapinzani wao.
Matokeo mengine Mbeya City imeondoka na pointi tatu baada ya kuilaza Kagera Sugar kwa bao 2-0 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Azam FC yenyewe iliendelea kujikita katika nafasi ya pili baada ya kuisambaratisha Stend United kwa ushindi wa bao 4-0 katika Complex, Chamazi,jijini Dar es Salaam.
kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 45 baada ya kucheza michezo 23, ikiwa nyuma ya Yanga SC yenye pointi 52 za mechi 23 na mbele ya Simba SC yenye pointi 41huku ikiwa imecheza mechi 24.
Mabao ya Azam yaliwekwa kimiani na Gaudence Mwaikimba aliyepaachika bao mbili pekee yake wakati, Farid Malik na Mshambuliaji kutoka nchini Uganda Brian Majwega wakifunga bao moja moja.
0 comments:
Post a Comment