BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

VYAMA VITAKAVYOVUTWA NA SERIKALI VYATAJWA.

 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe.

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakati wowote wiki hii itaanza kutoa orodha ya vyama vya kijamii vitakavyofutwa kwa kuanzia na mkoa wa Dar es Salaam.


Imesema vyama hivyo vitafutwa kutokana na kutotekeleza matakwa ya kisheria ya kuwasilisha taarifa za mwaka za ukaguzi wa hesabu za vyama na vile ambavyo havilipi ada ya mwaka kama sheria inavyoelekeza.

Msemaji wa wizara hiyo, Isaac Nantanga alisema hayo jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kufafanua suala la uhakiki wa vyama vya kijamii nchini.

Alisema vyama vitakavyobainika vitafutwa katika Daftari la msajili wa vyama vya kijamii na wala siyo Taasisi zisizo za kiserikali (NGO,s) kwani haihusiki nazo.

“Orodha ya vyama vitakavyofutwa itaanza kutolewa kwa awamu kuanzia wiki hii na kwa kuanzia orodha hiyo itahusu vyama vilivyosajiliwa mkoa wa Dar es Salaam”Alisema kufuatana na orodha iliyopo vyama 10,000 vya kijamii na Taasisi za Dini vimesajiliwa na wizara hiyo na vitakavyofutwa ni vile tu ambavyo haviwasilishi taarifa za kila mwaka za ukaguzi wa hesabu zao na pia kama havilipi ada ya kila mwaka kama sheria inavyotaka.

Juzi,gazeti moja la kila siku liliandika kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Mathias Chikawe anaanza kuhakiki NGOs jambo ambalo siyo la kweli kinachofanyika ni kwa taasisi za kijamii.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: