BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WALIOJITOKEZA KUGOMBEA URAIS KATIKA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 2015 NDANI YA CCM WAENDELEA KUBANWA MBAVU.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiCUkacGgKyDrbIsonrVxb8qLazQOsuUNuDWCzXJB93RcYPGF9mskGV6QIJYQEYAECsUMyjDLbWnpFrxBt64FeGu2NdvUr54HV2jMKh14g-Qq78lxuO4JFlLaSTgTd5jIIiKUxXuNgFMiM/s1600/7+(1).jpg
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimewataka viongozi wake walioanza kuwatembeza watu wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu, kuacha mara moja kwa kuwa wanakiuka kanuni za viongozi na maadili.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula alisema hayo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na wanachama, katika ziara yake kwenye majimbo ya Ukonga na Segerea.

“Kiongozi wa chama haruhusiwi kumtembeza mgombea au kumtambulisha kwa wanachama na ukifanya hivyo ni makosa,”alisema. Alisema muda utakapowadia, watu wanatakiwa kuchagua kiongozi kulingana na wanavyoona anafaa na si kwa kushawishiwa au kutumia pesa.

“Ni marufuku mgombea kuzungumza au kukutana na kamati ya utendaji kuanzia ngazi za chini kwa madai kwamba wanajitambulisha na kutoa nauli, ukibainika kufanya hivyo jina lako litaenguliwa,” alisema.

Alisema CCM imekuwa ikifuata kanuni na katika Uchaguzi uliopita walichukua hatua mbalimbali kwa waliozikiuka, ikiwemo kufuta majina na kuanza upya mchakato baada ya kugundua kuna waliokuwa wakisambaza fedha.

Aidha, Mangula aliwataka kutokukubali watu wanaovuruga amani na wasiozingatia taratibu, kwa kuwa machafuko yanapotokea, wanaoathirika siyo wanaoanzisha, bali ni wananchi wote.

“Kungekuwa hakuna amani, hakuna yeyote ambaye angeweza kukimbilia miradi au shughuli zake za maendeleo bali kila mtu angeangalia jinsi ya kujiokoa hivyo tuilinde amani tuliyonayo,” alisema.

Karipio la CCM limekuja huku chama hicho kikiwa kimeonya na kuadhibu baadhi ya makada wake walionyesha nia ya kuwania uongozi katika nafasi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Urais, wakidaiwa kupigana vikumbo vya chini kwa chini katika harakati za kutaka kupitishwa na chama ili kumrithi Rais anayemaliza muda wake, Jakaya Kikwete.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: