BAADA ya mpira
kumalizika katika uwanja huu wa Taifa klabu ya Yanga Afrika
imekabidhiwa kombe la ubingwa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuibuka na ushindi mnono bao 4 - 1 dhidi ya Polisi Moro katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Ushindi huu
umeiwezesha Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mapema ikiwa
na mechi 2 mkononi dhidi ya Azam FC na Ndanda FC kwa kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na
timu yoyote na kuivua ubingwa Azam FC.
Katika ushindi huo umechangiwa na mabao ya Magoli ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji, Amiss Jocelyn Tambwe aliyepachika bao tatu pekee yake wakati mshambuliaji mwenzake anayeongoza kwa kupachika mabao katika ligi hiyo, Simon Msuva akifunga bao moja.
Kwa Yanga kuondoka na ushindi wa bao 4 wakati Polisi Moro SC wakifunga bao 1, Mtanda Blog inatoa pongezi za dhati kwa klabu ya Yanga SC kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara katika msimu wa mwaka 2014/2015 sambamba na wanachama, mashabiki na wadau wanaoipenda klabu hiyo.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / michezo
/ YANGA SC YATWAA UBINGWA WA LIGI KUU TANZANIA BARA NA KUKABIDHIWA KOMBE UWANJA WA TAIFA DAR ES SALAAM.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment