BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ASKARI POLISI SITA WASHTAKIWA NA BARAZA KUU LA MAHAKIMU JUU YA KIFO CHA KIJANA ALIYEFARIKI DUNIA MIKONONI MWAO.

http://gdb.voanews.com/471752DB-DEB9-47D9-93BB-E47C6C8A77DE_w443_h249.jpg

Mwendesha mashitaka mkuu wa jimbo la Maryland nchini Marekani amesema kuwa maafisa wote sita wa jeshi la Polisi wanaoshitakiwa kwa kifo cha kijana Mmarekani mweusi aliyefariki mikononi mwao wameshitakiwa na baraza kuu la mahakimu.


Meya wa Baltimore Stephanie Rawlings-Blake akizungumza na waandishi wa habari huko Baltimore, Mei 1, 2015.

Mwanasheria mkuu wa jimbo Marilyn Mosbi alisema kuwa baraza kuu la mahakimu limeamua kwamba kuna kila sababu za kutosha za kuwafungulia mashitaka rasmi maafisa hao wa idara ya Polisi ya Baltimore kwa kumkamata Freddie Gray, ambaye alifariki dunia mwezi Aprili baada ya kujeruhiwa akiwa mikononi mwa Polisi.

Katika mkutano na waandishi wa habari Alhamisi Mosby alisema kuwa baraza la mahakimu limewasilisha mashitaka kadhaa dhidi ya Polisi wote sita na kuthibitisha shitaka kubwa kuliko yote la kitendo cha mauaji bila ya kudhamiria dhidi ya dereva wa gari la Polisi lililomsafirisha Gray baada ya kukamatwa Ceaser Goodson.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: