BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMATI KUU YA CCM YAWAONYA MAKADA WALIOPEWA ADHABU, NI WALE WALIOTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS DODOMA.

Kamati kuu ya chama cha mapinduzi CCM imekutana mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti rais Jakaya Kikwete ambapo miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni kupokea taarifa ya kamati ya usalama na maadili.

 
Katika kamati hiyo imeridhia pendekezo la kamati ya kumalizika kwa adhabu kwa makada sita waliotangaza nia ya kuwania urais lakini kikiwatahadharisha kuzingatia kanuni na maadili ya CCM.

Kamati hiyo imekutana mjini Dodoma ikiwa ni kikao kinachotajwa kuwa ni cha kwanza kwa CCM kuelekea katika kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu huku idadi ya wajumbe walioshiriki ikiwa ni 30 kati ya wajumbe 32 wa kamati kuu kama anavyofafanua katibu mkuu wa CCM Abrahmani Kinana.

Muda mfupi baada ya kufunguliwa kwa kikao hicho katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye alieleza kuwa miongoni mwa yanayojadiliwa kwa awali ilikuwa ni pamoja na kuwaasa wagombea wanaotajwa kukiuka miiko na maadili ya chama hicho kwa kufanya matendo yanayoonekana kuwa ni kampeni wanaweza kuondolewa katika uteuzi wa wagombea hasa katika nafasi kubwa ya urais. ITV
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: