Mshambuliaji wa timu ya soka ya kanda ya SUA, Fidoline Chendi akitafuta mbinu za kuwatoka walinzi wa timu ya kanda ya kati, Ally Katanga na Shakuru Maulid wakati wa mchezo wa fainali mashindano ya UMISETA ngazi ya kanda ya Manispaa ya Morogoro, Kanda ya SUA iliibuka na ushindi wa penalti 10-9 baada ya sare ya bao 1-1.
Juma
Mtanda, Morogoro.
Mashindano
ya kusaka wachezaji wenye vipaji ya umoja wa michezo kwa shule za sekondari
Tanzania (UMISETA) ngazi ya kanda ya Manispaa ya Morogoro yamemalizika kwa timu ya soka ya wavulana ya kanda
ya SUA ikitawazwa mabingwa kwa mwaka 2015 mkoani hapa.
Timu
ya soka kanda ya SUA chini ya kocha wao mkuu, Emmanuel Kimbawala maarufu kama Mourinho alilazimika kutumia kila aina ya mbinu ndani ya uwanja kwa mifumo tofauti
tofauti katika mchezo wa fainali dhidi ya Kanda ya Mjini Kati ili kuweza vijana wake kuibuka
kidedea kwa kupata ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penalti ya bao 11-10.
Katika
mchezo huo wa fainali timu ya soka ya Mjini Kati ndiyo iliyoanza kupata bao katika dakika ya
20 lililofungwa na mshambuliaji, Christopher Adam huku SUA wakilazimika kusawazisha katika dakika ya 90 kupitia
kwa, Michael Jeromeh na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mwamuzi
chipukizi wa mchezo huo, Raphael Ikambi aliamuru kupigwa penalti kama kanuni za mashindano hayo ili kupata
mshindi ambapo timu ya Mjini Kati ilipata penalti tisa wakati wenzao SUA wakipata penalti 10,
baada ya Joseph John kufunga penalti yao ya mwisho kufuatia, Abdul Shomari kukosa
penalti ya 10.
Kwa
upande wa soka la wasichana, kanda ya Tungi iliibuka mabingwa kwa changamoto ya
penalti baada ya kushinda penalti 2-1 dhidi ya Bigwa kufuatia kumaliza dakika
90 kwa sare ya 0-0.
Katika
mchezo wa netiboli, kanda ya Mjini Kati ilitwaa ubingwa huo baada ya kufikisha
pointi 10 na vikapu 130 ikifungwa vikapu 60 wakati katika mchezo wa wavu
wavulana kanda ya Tungi pia ilitwaa ubingwa huo wakati Kihonda A ikitwaa taji kwa
upande wa wasichana.
Kwa mchezo wa basketiboli, kanda ya Mjini Kati ilishinda taji baada ya kuilaza
Kihonda B kwa vikapu 44-39 katika mchezo wa fainali huku kwa mpira wa mikono
wavulana Kihonda B ilishinda taji hilo kwa kufikisha pointi tisa na wasichahana
kanda ya Mjini Kati ikitawazwa mabingwa.
Michezo ya UMISETA ngazi ya mkoa wa Morooro inatarajiwa kutimua vumbi Mei 27 mwaka huu katika uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
0 comments:
Post a Comment