BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA EDWARD LOWASSA JINA LAKE KUKATWA NA KAMATI KUU YA CCM KILICHOJITOKEZA USIKU WA NANE MJINI DODOMA NDICHO HIKI.


Habari kutoka makao makuu ya CCM mkoani Dodoma zinaeleza kuwa baadhi ya wajumbe watatu wa kamati kuu ambao ni Dkt. Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa wamepinga maamuzi ya kamati ya kumkata mmoja wa wagombea maarufu na kumweka mgombea asiyekuwa maarufu.


Akizungumza jana waandishi wa habari usiku wa kumkia leo majira ya saa saba, Dkt. Nchimbi alisema kwamba wao watatu hawajakubaliana na maamuzi ya kamati kuu iliyoketi usiku huo chini ya Mwenyekiti Dkt Jakaya Kikwete kumkata mgombea maarufu kwa manufaa ya mgombea asiye maarufu.

“Katika kikao cha leo (jana) kamati haikupoea majina yote yaliyojadiliwa na maadili, suala ambalo ni kinyume na kanuni, pili katiba ya CCM inataka mtu anayekubalika ndiye apewe nafasi ya kwanza, lakini kikao cha jana kimeonyesha kuminya wanaokubalika kwa manufaa ya wachache wasiokubalika” Alisema Dkt. Nchimbi.

 
 Hta hivyo kwa sababu hiyo, wao watatu ambao ni wajumbe wa kamati kuu wamewataarifu wenzao kwamba wamejitenga na maamuzi ya kikao hicho na kutangaza kutoyaunga mkono.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania zinaonesha kuwa mgombea anayekubalisa sana CCM ni Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akifuatiwa na Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe.

Hapo chini nimekuwekea Video ya Emmanuel Nchimbi akiyapinga maamuzi hayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: