Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Monduli, Joseph Silonga, ametangaza kujivua wadhifa wake kwa kile alichodai kutemwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Monduli baada ya kushinda kura za maoni.
Alisema uongozi wa juu wa chama hicho umemtema jina lake akiwa mshindi wa kwanza wa kura za maoni za ubunge wa Jimbo la Monduli, na badala yake umemteua mshindi wa pili.
Akizungumza na waandishi wa habari Monduli jana, Silonga pamoja na Katibu Mwenezi wa Wilaya hiyo, Patrick Ole Mrugi na wajumbe wao 15 walisema wanajivua nyadhifa zao lakini wataendelea kuwa wanachama.
“Mimi nilikuwa mshindi wa kwanza katika kura za maoni lakini chama changu kimemtangaza mshindi wa pili, Joseph Kalanga diwani wa CCM aliyehamia Chadema hivi karibuni kuwa mgombea ubunge.
“Sijapewa taarifa kwa nini nimetemwa, chama hakijatoa tamko rasmi,” alisema.
“Nimetumia muda wangu mwingi kukijenga Chadema jimboni humu, na hata katika uchaguzi wa udiwani uliopita katika katika Kata ya Mto wa Mbu nilishinda lakini jina langu likakatwa kimizengwe,” alisema.
Alisema hajaridhika kwa namna yoyote, na anatamka kwamba anajivua wadhifa wake na ataendelea kubaki kuwa mwanachama.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / siasa /
slider
/ MGOMBEA URAIS KUPITIA UKAWA EDWARD LOWASSA APATA PIGO LA KWANZA NYUMBANI KWAKE MUNDULI.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment