Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
VURUGU kubwa zimetokea kwenye Ofisi za CHADEMA, Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, baada ya wafuasi wa chama hicho, kupinga uteuzi wa mgombea ubunge jimboni humo, Hamis Mwagao.
Wafuasi waliopigana mbele ya ofisi za chama hicho ni wale wanaomuunga mkono Mwagao na wafuasi wa mgombea aliyeongoza kwenye kura za maoni Fransisco Shejamabu, ambaye aliachwa katika uteuzi huo.
Vurugu hizo zilianza juzi mchana baada ya Mwagao kutangazwa kuwa ndiye mgombea ubunge wa jimbo hilo na Shejamabu kuachwa, hivyo kusababisha hasira kwa baadhi ya wafuasi ambao waliandamana hadi kwenye ofisi za CHADEMA kupinga uteuzi huo.
Walipofika katika ofisi hizo, ndipo wakaanza kushikana mashati, kupigana ambapo baadhi ya viongozi wa chama hicho waliokuwepo katika ofisi hizo, waliingilia kati na kutuliza ghasia hiyo.
Wakizungumzia sitofahamu hiyo, mmoja wa wafuasi hao, Paskali Kingi (31) anayemuunga mkono Shejamabu, alisema mgombea huyo ni kiongzi mwenye hekima na msomi hivyo angeweza kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya jimbo hilo.
Godfrey Kazimili (30) anayemuunga mkono Mwagao, alisema mgombea huyo ana rekodi nzuri ya uongozi tangu akiwa diwani kupitia CCM kabla ya kuhamia CHADEMA.
Katibu wa CHADEMA jimboni humo, Boniface Mafuru na Katibu wa chama hicho Wilaya, Mashauri Deusdedith, kwa nyakati tofauti, wamekiri kuwepo kwa tukio hilo.MAJIRA
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / siasa /
slider
/ WANA CHADEMA WATWANGANA MAKONDE MAZITO OFISI ZA CHAMA KUPINGA UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment