BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BAADA YA KIFO CHA WAZIRI CELINA KOMBANI, SERIKALI YATAJA SABABU NA KUZIKWA MAHENGE MOROGORO.


Usiku wa September 24 2015 taarifa ya Majonzi imesambaa na kuwafikia watu kupitia Vyombo mbalimbali vya Habari pamoja na mitandao ya Kijamii.


Serikali ikathibitisha pia kuhusu msiba wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mama Celina Kombani amefariki Dunia kutokana na maradhi ya Saratani, na amefariki akiwa India ambako alienda kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kuhusu taratibu zinazofatia, nimeipata taarifa kutoka Ofisi za Bunge ambapo inaonesha mipango ya kusafirisha mwili wa Marehemu mpaka Dar es Salaam inafanyika na mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Dar Jumatatu September 28 2015, na baadae msiba utasafirishwa kupelekwa Mahenge Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya mazishi.

Marehemu Mama Celina Kombani amefariki akiwa na umri wa miaka 56 na alikuwa Waziri na pia Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki.

Makamba na Kabwe ni miongoni mwa watu waliostushwa na tukio hilo la kifo cha kiongozi huyo.

Mpenzi wetu Celina Kombani, Mbunge wa Ulanga Mashariki, hatunaye tena. Bwana ametoa, bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Pumzika kwa amani.
 

Nimepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya msiba wa Mama Celina Kombani. Nawapa pole wananchi wa Ulanga Mashariki na Chama. Posted by Zitto Kabwe
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: