ENDAPO RUNGWE AKACHAGULIWA KUWA RAIS BAADA YA UCHAGUZI MKUU, WAKUU WOTE WA MIKOA NA WILAYA KUPIGWA CHINI KISHA KUANZISHA SERIKALI YA MAJIMBO.
Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashimu Rungwe.
Mgombea urais kupitia tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashimu Rungwe, amesema endapo chama chake kitapata ridhaa ya kuongoza nchi kitahakikisha kinawaondoa wakuu wa mikoa na wilaya, na kuanzisha serikali ya majimbo.
Akizungumza jana kwenye kampeni zake za kuwania urais, uliofanyika kwenye kituo cha mabasi ya zamani mjini Shinyanga, Rungwe alisema wakuu wa wilaya na mikoa wamekua kero kwa wananchi kwa kuwa hawachaguliwi bali wanateuliwa na rais, na kwamba wamekuwa wakitumikia sera ya chama hicho kilicho wachagua.
Sera ya Chaumma kama tutapa ridhaa ya kuongoza Serikali ya Tanzania lazima tutawaondoa wakuu wa mikoa na wilaya, kwani ndio watu wanaochangia wananchi kutokuwa na maendeleo na kubaki na wimbi la umaskini,î alisema Rungwe na kuongeza kuwa.
Viongozi hawa wamekuwa wanafanya wanavyotaka kwa sababu wananchi hawajawaweka kwenye nafasi hizo, Sasa Chaumma itaanzisha serikali ya majimbo vyama vyote vishiriki kugombea nafasi hizo, kwa kufanya hivyo watawathamini wananchi, kwani wao ndio watakua wamewaweka madarakani na wanauwezo wa kuwaadhibu.
Pia alizungumzia suala la kuanzisha kilimo cha kisasa, ambapo alisema atatumia teknolojia ya umwagiliaji kwa kutumia ndege, ili wananchi waweze kulima mazao mengi na kukabiliana na baa la njaa ambalo limekuwa likiwakabili kila mwaka na kutotegemea msaada kutoka nje ya nchi.
Alisema nchi inauwezo wa kufanya hivyo, na sasa ni wakati wa wananchi kufanya mabadiliko na kuiondoa Serikali ya CCM ambayo imeshindwa kufikilia jambo hilo kwa muda wote iliyotawala, na kwamba Chaumma kikipata nafasi hiyo itaonesha kuwa inaweza kubadilisha maisha ya Watanzania.
Naye Mgombea mweza kupitia chama hicho Issa Abasi Hussein aligusia suala la Elimu na kusema wao wakishika madaraka elimu itakua bure kuanzia Chekechea hadi Shahada ya kwanza, ikiwa enzi za ukoloni watu walisoma bure kwanini leo ishindikane kwa serikali yao ya Chaumma.
Pia Hussein aliahidi wakazi wa mkoa wa Shinyanga endapo wakishika dola watahakikisha wanajenga viwanda vya ngozi na kusindika nyama, ikiwa mkoa huo unawafungaji wengi hali ambayo itatoa fursa kwa wananchi kupata ajira pamoja na kupunguza ukali wa maisha na kukua kiuchumi. CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment