Dar es Salaam. Wakati kasi ya maambukizi mapya ya Ukimwi ikipungua nchini, tafiti zimebainisha Jiji la Dar es Salaam linashikilia nafasi ya sita miongoni mwa majiji yaliyoathirika zaidi barani Afrika.
Takwimu hizo zipo kwenye ripoti ya utafiti uliofanywa na Shirika la Kimataifa la Wahamiaji (IOM) uliofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam na kuangalia namna jamii za watu wa maeneo ya bandari walivyo na uwezekano wa kupata maambukizi mapya ya ugonjwa huo kutokana na mwingiliano wa mataifa mbalimbali.
Mshauri wa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Ukimwi (UNAIDS), Marie Engel katika uwasilishwaji wa ripoti hiyo uliofanyika leo jijini Dar es Salam alisema ingawa maambukizi yamepungua nchini, bado Dar ni miongoni mwa majiji yaliyoathirika zaidi.
“Dar es Salaam ni jiji la sita kati ya 10 yaliyoathirika zaidi Afrika ikiwa na asilimia 6.2 za maambukizi mapya kwa mwaka. Maambukizi ya ndani yamepungua kwa kiasi na mpaka mwaka jana yalikuwa asilimia tano maeneo ya mjini na 7.2 vijijini huku wastani kwa nchi nzima ukiwa asilimia tano,” alisema Marie.
Alifafanua kwamba vita dhidi ya ugonjwa huo vinaendelea na kwamba jamii ya kimataifa inaamini mpaka mwaka 2030 utakuwa historia ingawa kuna kazi kubwa inahitaji kufanywa ili kufikia lengo hilo la kuukabili Ukimwi ulianza kuenea miaka ya 1980.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ JIJI LA DAR ES SALAAM LASHIKA NAFASI YA SITA KWA MAAMBUKIZI YA UKIWMI BARANI AFRIKA.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment