Umati wa waumini wa dini ya Kiislam waliokwenda
kuhiji Makka, Saudi Arabia.
Dar es Salaam. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa imepokea majina 18 kati ya 50 ya Mahujaji kutoka Tanzania ambao hadi sasa hawaonekani kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe wiki iliyopita na kusababisha vifo vya watu 769 na wengine 934 kujeruhiwa.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo inasema Mahujaji wa Tanzania wapatao 50 bado hawajaonekana huku wengine watano wakiwa wamefariki dunia.
Taarifa hiyo ya wizara imeyataja majina hayo yaliyopatikana hadi sasa kuwa ni Abdul Iddi Hussein, Awadh Saleh Magram, Burhani Nzori Matata, Yussuf Ismail Yusuf, Saleh Mussa Said, Adam Abdul Adam na Archelaus Antory Rutayulungwa.
Wengine ambao majina yao yamepatikana huku ikiwa bado hawajulikani walipo ni Farida Khatun Abdulghani, Rashida Adam Abdul, Hamida Ilyas Ibrahim, Rehema Ausi Rubaga, Faiza Ahmed Omar, Khadija Abdulkhalik Said, Shabinabanu Ismail Dinmohamed, Salama Rajabu Mwamba, Johari Mkesafiri Mwijage, Alwiya Sharrif Salehe Abdallah na Hafsa Sharrif Saleh Abdallah.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mbali na taarifa za kupatikana kwa majina hayo, wizara imepokea taarifa ya kutambuliwa kwa mwili wa hujaji mmoja wa Tanzania aliyetambulika kwa jina la Hadija Shekali Mohammed wa kikundi cha Ahlu Daawa”.
Imeongeza kuwa Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha za maiti za Mahujaji waliofariki Makkah ambao wamehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti kwa ajili ya utambuzi na kwamba ubalozi wa Tanzania nchini humo kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission pamoja na vikundi vya Mahujaji wanaendelea na zoezi la kuzihakiki picha hizo ili kubaini kama zinalingana na sura za Mahujaji wetu waliopotea.MWANANCHI
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ MAJINA 18 TU NDIYO YALIYOPATIKANA KATI YA MAHUJAJI 50 WALIOPOTEA KWA TANZANIA KATIKA IBADA YA HIJA MINA MAKKAH..
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment