Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter akihutubia katika moja ya mikutano ya chama hicho.
Mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mchungaji Peter Msingwa na wafuasi 67 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu ambazo hazijafahamika hadi sasa.
Taarifa kutoka mkoani Iringa zinapasha kuwa, wafuasi hao walikuwa kwenye kikao cha siri jana usiku majira ya saa saba katika moja ya hoteli.
Imeelezwa kuwa mgombea huyo kupitia Chadema alikuwepo kwenye mkutano huo lakini aliondoka kabla ya polisi kuvamia hoteli hiyo na kuwakamata wafuasi hao wasiopungua 67.
Hata hivyo, mbunge huyo aliyemaliza muda wake na ambaye anawania tena kiti hicho Iringa Mjini aliunganishwa na kundi hilo la wafuasi na sasa wako chini ya ulinzi.
Wakati huohuo, wafuasi wa Chadema wakiongozwa na kada Ester Bulaya wamekusanyika katika mahakama ya wilaya ya Bunda, mkoani Mara leo wakitaka wenzao watatu kuachiwa kwa dhamana.
Ester Bulaya anayegombea ubunge kupitia Chadema pamoja na wafuasi wa chama hicho wamewasili mahakamani hapo leo asubuhi kwa utulivu huku wafuasi wakitaka wenzao wanaotuhumiwa kwa unyang’anyi kwa kutumia silaha waachiwe.
Wafuasi hao wanaotuhumiwa kwa unyang’anyi, walikamatwa wiki iliyopita pamoja na gari la Bulaya ambalo wakereketwa wa chama hicho cha upinzani wanataka polisi waliruhusu ili liendelee na shughuli za kampeni.MWANANCHI DIGITAL
0 comments:
Post a Comment