BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UKAWA KUMEKUCHA !: CUF NA CHADEMA WAKUNJANA MASHARTI KATIKA MKUTANO WA KAMPENI DAR ES SALAAM.

Dar es Salaam. Wafuasi wa vyama vya Chadema na CUF wamekunjana mashati kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Ukawa uliofanyika Uwanja wa Barafu, Mburahati, Dar es Salaam.

Sakata hilo lilianza kwa kila upande kurushiana kauli za kuudhi baada ya wanachama wa CUF kupokonywa mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kumkataa mgombea udiwani wa Chadema, Hemed Sabula.

Tukio hilo lilitokea saa 10:00 jioni, dakika chache kabla ya kuanza kwa mkutano huo.

Kata ya Mburahati ina mitaa mitatu ya Barafu, Kisiwani na NHC huku yote ikishikiliwa na CCM katika nafasi ya udiwani.

Pamoja na hali hiyo, Mwenyekiti wa CUF wa kata hiyo, Kazi Kalesela alisema mgombea wao ndiye mwenye sifa za kuwania kata hiyo kwa kuzingatia vigezo vya Ukawa.

“Matokeo ya serikali za mitaa CUF ilishika nafasi ya pili kwa mitaa yote, 2010 pia mgombea udiwani wa CUF alishika nafasi ya pili,” alisema. Hata hivyo Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) wa kata hiyo, Shaaban Kipingu alisema viongozi wote Ukawa ndani ya kata hiyo walisaini makubaliano ya kumsimamisha mgombea wa Chadema, Sabula.

“Makubaliano yaliyoletwa na mgombea ubunge, Said Kubenea kuhusu kata za Ubungo ni kwamba, kata tano ikiwamo hii ziende Chadema na tatu ziende CUF. Alisema hata utambulisho wake umefanyika wakati wa uzinduzi wa kampeni za jimbo zilizofanyika Ubungo, lakini tatizo lililopo ni usaliti wa wanachama na fitina.

Katika mkutano huo, Duni alifunga mkutano bila kumtambulisha diwani yeyote kati yao na badala yake alimtambulisha mgombea ubunge wa Ubungo, Kubenea.

Duni aliwataka Watanzania kuchagua Ukawa kwa ajili ya kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali za maendeleo kwa kuwa CCM imeshindwa kuwasaidia kufikia malengo yao.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: