WANAWAKE TISA WAKAMTWA KWA KUTISHIA AMANI KATIKA KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU MKOANI MBEYA
Picha ya maktaba akionekana mwanamke akiwa na pingu mkononi.
Mbeya. Watu 41 wakiwamo wanawake tisa wamekamatwa mkoani hapa kwa tuhuma za kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali wakati wa kampeni zinazoendelea kuwanadi madiwani na wabunge.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Ahmed Msangi amesema hayo leo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu tathimini ya matukio ya uchaguzi.
Amesema tangu kampeni zilipoanza matukio 30 ya uhalifu yalifanyika yakiwahusisha wanaume 32 na wanawake tisa.
Amesema tukio moja kati ya hayo lilimhusisha Aman John ambaye amefikishwa kortini na kupatikana na hatia iliyosababisha alipe faini ya Sh30,000.
“Kesi nane kati ya matukio hayo zipo mahakamani zikiwa katika hatua mbalimbali lakini kesi tatu majalada yapo ofisi ya wanasheria wa Serikali wakati kesi zingine 19 zinapelelezwa,’’ amesema.
Amesema waliokamatwa wametuhumiwa makosa mbalimbali yakiwamo ya kuchana mabango ya wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani.
‘’Wengine wamekamatwa kwa makosa ya kung’oa bendera, kuharibu mali, kufanya fujo, kujeruhi, kuingilia mkutano, kutishia kuua kupigana hadharani na wizi’’ amesema kamanda huyo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment