
Mshambuliaji wa Burkina FC, Salum Machaku akiwatoka walinzi wa Kurugenzi Mufundi FC, Brown Chalamila kulia na Dotto Maloda wakati wa mchezo huo ambapo Burkina FC ilifungwa bao 2-1 katika uwanja wa jamhuri Morogoro. PICHA/Juma Mtanda
Na Juma Mtanda.
Kikosi cha timu ya soka ya Burkina FC ya Morogoro kimendelea kufanya vibaya ligi daraja la kwanza Tanzania bara baada ya kukubali vipigo mfululizo na kujikuta ikigawa pointi kwenye uwanja wake wa nyumbani mbele ya wapinzania katika michezo mitatno ya ligi hiyo iliyochezwa uwanja wa jamhuri mkoani hapa.
Vipigo hivyo vimeifanya timu hiyo kuambua pointi moja na kufungwa michezo minne mfululizo.
Ndoto za timu hiyo kupata ushindi ligi hiyo katika mchezo wa tano kwenye uwanja wa Jamhuri uliota mbawa baada ya Kurugenzi Mufundi FC kutibua mipango na kujikuta ikitandikwa bao 2-1.
Katika mchezo wa juzi (jana) dhidi ya Burkina FC na Kurugenzi Mufindi FC, mshambuliaji Burkina FC, Rajabu Twaha alifunga bao pekee dakika ya 44 kipindi cha kwanza akitumia vyema mpira wa adhabu ndogo uliochongwa na Omari Bambam na kuwababatiza walinzi wa Kurugenzi Mufundi FC kisha kukwamisha mpira nyavuni kiurahisi.
Dakika ya 55 George Mpole aliishawizishia Kurugenzi Mufundi kwa shuti kali nje ya 18 baada ya kunasa pasi ya ndugu yake kabla dakika 86 Miraj Mwilenga kufunga bao la pili na ushindi kwa kufumua shuti kali nje ya 18 kufuatia pasi ya George Mpole aliyefanya kazi kubwa ya kupangua ngome ya Burkina FC waliojikuta wakipoteza mchezo huo kwa mara ya tano.
Burkina FC katika ligi hiyo imefanikiwa kuambulia pointi moja kutoka kwa Kimondo FC ya Mbeya baada ya sare ya bao -1-1 na kukumbana na vipigo vinne kutoka kwa Polisi Moro SC iliyoibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa ufunguzi huku JKT Shooting ikipata ushindi wa bao 2-1.
Timu nyingine iliyotembeza kipigo kwa Burkina FC ni pamoja Njombe Mji FC iliyoondoka na ushindi wa bao 2-0.
Kutokana na mwenendo wa kundi A timu ya Njombe Mji FC imefikisha pointi 10 baada ya kuifunga JKT Mlale iliyobaki na pointi zake nane.
Timu ya Ruvu Shooting inayoongoza kundi hilo kwa pointi 10 ikiwafuatiwa Kurugenzi Mufindi na Polisi Moro SC zikikabana koo kwa kukusanya zikitofautiana idadi ya magoli ya kufungwa na kufunga.
Ligi hiyo itisimama kwa muda kupisha uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu na kuendelea tena Okotba 31.MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment