BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MCHUNGAJI CHRISTOPHER MTIKILA AZIKWA KIJIJI CHA MILO WILAYA YA LUDEWA MKOA WA NJOMBE.

 
Safari ya mwisho duniani ya aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, ilimalizika jana baada ya mwili wake kuzikwa katika kijiji cha Milo, wilayani Ludewa, mkoa wa Njombe na mazishi yake kuhudhuriwa na watu kutoka sehemu mbalimbali wakiongozwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi.

Wakati wa mazishi hayo ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Mtikila waligubikwa na simanzi kubwa na kuelezea hisia zao juu ya kifo cha mchungaji huyo.

Baadhi ya waombolezaji walisema taifa limepoteza mtu supavu na asiye na woga katika kupigania haki za Mtanzania na mwanasiasa ambaye hakuwahi kukata tamaa kutokana na ujasiri wake.

Akizungumza wakati wa mazishi hayo, Jaji Mutungi alisema wamefika kumsindikiza marehemu bila kuwa na itikadi ya chama chochote kwani Mchungaji Mtikila alikuwa ni kiongozi wa kitaifa wa chama na kiongozi shupavu.

“Watanzania kumeuenzi Mchugaji Mtikila ni kufanya yale aliyo kuwa akiyafanya na yanatimia, hakuwa mwoga kufuatilia jambo ambalo ana amini kuwa ni la kweli. Alikuwa hapendi njia za mkato Kupata jibu la kitu, alipenda mtu ajenge hoja,” alisema.

Jaji Mutungi aliwapa pole wanafamilia, wanachama wa DP na Watanzania kwa ujumla na kuwataka kuwa wavumilivu wakati huu wa kipindi Kigumu cha msiba na majonzi.

Aliwataka Watanzania kudumisha amani na upendo katika kipindi hiki cha uchaguzi ili kuepuka machafuko na Tanzania iendelee kuwa na umoja wa kitaifa.

Kwa upande wake, dada wa marehemu, Veronica Mtikila, alisema wamepoteza mtu muhimu katika familia na taifa kwani alikuwa ni mwanasiasa maafuru na mwenye msaada mkubwa kwa familia.

Mchungaji Mtikila alifariki Oktoba 4, mwaka huu katika eneo la Msolwa, mkoani Pwani baada ya gari alilokuwa akisafiria na watu wengine watatu kupata ajali wakati wakitokea Njombe kwenye kampeni za kumnadi mgombea wa ubunge wa chama hicho.


Marehemu ameacha mke bila watoto. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amina.CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: