BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA URAIS WA CCM AIVURUGA DODOMA NA KUWEKA HISTORIA

MGOMBEA urais wa CCM, Dkt. John Magufuli, jana ameanza kampeni zake mkoani Singida akitokea mkoani Dodoma ambako alifanya mikutano ya kampeni kwenye Wilaya za Mpwapwa, Kongwa, Chamwino na kuhitimisha kwa mkutano mkubwa uliofanyika Dodoma Mjini. 

Katika mikutano hiyo, Dkt. Magufuli alivitaja vipaumbele mbalimbali ambavyo atavitekeleza baada ya kuchaguliwa katika nafasi ya urais, kuingia Ikulu na kuunda Serikali. 


Alisema baadhi ya vipaumbele hivyo vipo katika Ilani ya CCM ikiwemo utoaji elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne, mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana ili waweze kuondokana na umaskini, kukuza vipato vyao na kumudu gharama za maisha. 


Aliahidi kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimeliangamiza Taifa, wizi na ufisadi ambavyo atavikomesha na kubaki kuwa historia katika uongozi wake. 


"Watanzania wana kilio kikubwa katika maeneo haya kila kukicha, mimindiye Dkt. Magufuli ambaye nitakomesha vitendo hivi," alisema mgombeahuyo ambaye katika mikutano yake haachi kuhubiri amani na kuahidikuwatumikia Watanzania usiku, mchana ili kuharakisha maendeleo. 


Alisema atajenga uhusiano mzuri na wafanyakazi, kuboresha masilahiyao ili waweze kufanya kazi kwa raha na moyo wa kizalendo kwa manufaa ya Watanzania. 


"Baadhi ya mafisadi, wezi wameanza kukimbia baada CCM kuniteuakuwa mgombea urais lakini nikiingia Ikulu, nitawafuata huko waliko ili niwashughulikie vizuri ndiyo maana maana nimesema nitaunda mahakama ya Mafisadi," alisema Dkt. Magufuli.majira
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: