BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA WA URAIS WA CCM DK MAGUFULI AANZA KUMWAGIWA SIFA KABLA YA NDOTO YA KUINGIA IKULU.

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli
 
MGOMBEA urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein, amesema mgombea urais wa chama hicho wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli, mbali na uchapakazi wake, ni mtu anayependa ushirikiano.

Dk Shein amesema hayo jana katika mkutano wake mkubwa wa kampeni mjini Zanzibar na kusisitiza kuwa Tanzania bado inastahili kuongozwa na viongozi kutoka chama hicho.

“Ni kiongozi mchapakazi kazi, uchapakazi wake unafanana na tabia yake ya kupenda kwake kazi na anapenda ushirikiano na wenzake na sisi tunaamini huyu ndie Rais wetu ajaye wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,” amesema Dk Shein huku akishangiliwa na umati wa watu.

Dk Shein ameuambia umati wa wananchi waliohudhuria kuwa CCM hakina mbadala nchini Tanzania na kwamba wagombea wengine katika Uchaguzi Mkuu watabaki kuwa wasindikizaji.

Mgombea huyo, ambaye pia ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), aliahidi akichaguliwa atashirikiana na kushauriana na Dk Magufuli katika kuongoza Tanzania kama wanavyofanya sasa yeye na Rais Kikwete na kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa moja yenye amani na utulivu na kuendeleza Muungano wake.

Aliwataka wananchi kumchagua Dk Magufuli ili awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba wakimchagua atakuwa ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama.

“Mkimchagua Dk Magufuli atakuwa ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hivyo atatuhakikishia ulinzi wa nchi yetu na Muungano wetu,” alieleza Dk Shein.

Alimsifu Dk Magufuli kuwa kiongozi mwenye sifa zote zinazostahiki kuongoza Tanzania na kuwa chini ya uongozi wake Tanzania itaendelea kuwa salama salimini. Aliwaeleza wananchi kuwa Dk Magufuli amekuwa Waziri muda mrefu akiongoza wizara mbali mbali hivyo ana uzoefu mkubwa wa uongozi serikalini na anaijua vyema serikali.

Aliongeza kuwa Dk Magufuli ni muumini mzuri wa Muungano na anaujua vyema na kwamba amefanya kazi nzuri kuimarisha Muungano huo wakati akitekeleza majukumu yake aliyokuwa nayo. Kwa hivyo Dk Shein aliwataka wananchi kuwachagua wagombea wa CCM akiwemo yeye na Magufuli ili kuuweka uongozi wa Tanzania chini ya mikono ya CCM.

Dk Magufuli Akizungumza katika mkutano huo, Dk Magufuli aliahidi kulinda muungano kwa nguvu zake zote, huku akielezea namna anavyomfahamu Dk Shein tangu alipokuwa Makamu wa Rais wa Awamu ya Tatu, mpaka Makamu wa Rais katika miaka mitano ya kwanza ya Serikali ya awamu ya nne.

Dk Magufuli alielezea kushangazwa na wapinzani wanaosema kuwa hakuna kilichofanyika na kuhoji hata katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume, hawaoni kilichofanyika ingawa kila mara wanakitumia, huku akiahidi kuendeleza utalii na kuboresha shughuli za uvuvi.HABARILEO
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: