Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Jeti Lumo, Dar es Salaam jana, alisema hizo taarifa hizo si za kweli na ni uzushi.
“Mimi kama mwana familia nakanusha taarifa hizo zinazosambaa mitandaoni, habari hizo hazina ukweli hata kidogo.
“Jenerali Mwamunyange ni mzima wa afya, anaendelea na shughuli zake kama kawaida na yuko nje ya nchi kwa safari za kazi,” alisema Aden.
Alisema ni kawaida kwa Jenerali Mwamunyange kumuaga kila anaposafiri na kama kaka yake alimuaga kuwa alikuwa anasafiri kikazi kwenda nje akianzia Italia.
Pia alikanusha taarifa zilizosema kuwa ukoo wao umepewa fedha kuzima taarifa za Jenerali Mwamunyange na akawataka wananchi kuzipuuza.
0 comments:
Post a Comment