
"Baba yangu Capt.William Silaa akiwa na Mhe, Deo Filikunjombe na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya helicopter 5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa. Taarifa za mwisho ilionekana imeanguka kwenye msitu wa Selous. Hakuna mawasiliano ya simu.

Kutokana na tukio hilo vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali usiku kucha wa jana kuamkia leo viliendelea na jitihada za kufika eneo la tukio na jitihada kubwa zaidi ziliendelea.
Ajali hiyo imetokea katika kitalu cha wawindaji kinachojulikana kama R3 ambapo walioshuhudia wakiwa katika kitalu R2 tofauti yao ni kwamba wametenganishwa na mto ambao maji yake yanaenda kwa kasi huku kukiwa mamba"alisema Waziri Nyalandu.
“Sisi tulichokifanya kama Serikali ni kwamba tumetuma kikosi kimoja ambacho kilikuwa kina askari nane huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paulo naye akituma askari kwenda kwenye eneo hilo la ajali.
Taarifa ya awali ya tukio hilo baada ya waziri kupata taarifa ilieleza kuwa....“Taarifa tulizozipata kutoka kwa mashuhuda wa eneo hilo kwa wawindaji mahiri walipiga simu kwa njia ya Satelite na kueleza kuwa wameona helikopta moja imeaguka katika msitu wa Selous kwenye kitalu R3 jirani na mto Ruaha baada ya hapo kisha wakaona moto ukiwaka.”alisema Nyalandu katika taarifa yake fupi.Chanzo Millardayo.com
0 comments:
Post a Comment