Wajasiliamali zaidi ya 1070 kutoka sekta isiyo rasmi wameuomba mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF kuangalia upya masharti ya utoaji wa mafao yanayotolewa kwa wanachama wake baada ya kujiunga hasa kwa wanachama waliopo kwenye mfumo huo hapa nchini.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya namna ya kujiunga uanachama katika mfuko huo wa hifadhi ya jamii wa PPF kupitia mafao ya mfumo wa Wote Scheme mjini Morogoro jana, walisema kuwa mfuko huo kupitia kwa watalaamu wake wanapaswa kuangalia upya masharti ya utoaji wa mafao ili yaweze kumnufaisha mwanachama mapema.
Mafao ya Wote Scheme yana lenga la kumnufaisha mwanachama kutoka sekta isiyo rasmi pia ikiwanufaisha na wale wanachama waliopo katika sekta rasmi.
Baadhi ya maafisa wa mfuko wa hifadhi ya jamii kanda ya mashariki na kati (PPF) wakiwa jazia fomu za kujiunga na mfuko huo wakati wa mafunzo ya namna ya kujiunga na mfuko huo kupitia mfumo wa Wote Scheme wenye mafao matano yakiwemo ya kutibiwa bure kupitia Mfuko wa Taifa waBima ya Afya (NHIF) yaliyowashirikisha wajasiliamali zaidi 1070 mkoani Morogoro.
Mafao hayo ni pamoja na afya (Jali afya yako na PPF), Fao la Uzeeni (Staafu na PPF), Mkopo wa Elimu (Kopa na Ujiendeleze kielimu na PPF) na Mkopo (Kopa na Utimize ndoto yako na PPF).
mmoja wa wajasiliamali akitichangia mada wakati wa uzinduzi huo, Samuel Mlali (51) alieleza kuwa ana imani kubwa kuwa mfumo huo imelenga kuwasaidia watu wenye kipato duni baada ya kujiunga kwa kunufaika na mafao hayo hasa katika suala zima la afya, elimu, fao la uzeeni na mikopo lakini baadhi yake yanachukua muda mrefu mwanachama kunufaika nayo.
“Ningeulizwa hii leo na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF kwa muda gani wa mwanancha aanze kupata mafao haya baada ya kuanza kuchagia ?, jibu ningesema aanze kunufaika nayo baada ya miaka mitato badala ya miaka 15 iliyowekwa na PPF.”alisema Mlali.
Mlali alisema kuwa muda uliowekwa kwa baadhi ya kuanza kupata mafao hayo ni mrefu kutokana na wengi wanaochangia katika sekta isiyo rasmi kujikuta wana umri wa kuanzia miaka 35 hadi 45 na mfuko unawataka kuanza kupata baadhi ya mafao awe amefikisha kuchangia miaka 15 baada ya kujiunga hasa kwa kuangalia muda wa kustaafu ni miaka 55 hadi 60 kwa lazima.
Kwa upande wa Martha Kahaya (42) kutoka kikundi cha Hakuna Matata alisema kuwa amefurahishwa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF kwa kuingiza wanachama wanaochangia kwa hiyari kupata mafao yatakayosaidia kupunguza changamoto za lazima.
Msimamizi wa kanda ya mashariki na kati kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii PFF, Agnes Kakwi alisema kuwa uzinduzi huo umeshirikisha wanachama 1080 kutoka kwenye vikundi vya wajasiliamali vya Hakuna Matata, Save Family na Image Tanzania.
Kakwi alisema kuwa lengo la uzinduzi huo kwa wajasiliamali kutoa elimu juu ya mafao yanayotolewa na PPF baada ya mwanachama kujiunga.
“Kwa mfuko wa PPF kwa kanda ya mashariki na kati hapa Morogoro leo ndiyo tumezindua mfumo maalumu wa kuchangia unaozihusisha sekta isiyo rasmi na lengo kuu kuona jamii hiyo inatufaika na mafao hayo matano ambayo kimsingi yanachangamoto kutokana na hali halisi ya kipato.”alisema Kakwi.
Kakwi alisema ukiangalia baadhi ya faida ya mafao ya PPF ni pamoja na kupata matibabu ya afya kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) sambamba na fao la elimu analoweza kufaidika nalo mzazi kwa kupata mkopo wa elimu.CHANZO:MTANDA BLOG
0 comments:
Post a Comment