Ratiba ya Kuaga kwa MWILI wa Kipenzi chetu Deo Filikunjombe na wapendwa wetu wote Casablanca Haule, Egid Nkwera Ktk Safari yao ya Mwisho:-
Saa tatu Kitaifa Lugalo Hospital ya Jeshi
Saa Tano Nyumbani Kwa Mbunge Deo Filikunjombe, Mtoni Kijichi
Safari LUDEWA saa 6:30.
Jina la Bwana Lihimidiwe
. Deo Filikunjombe kamaliza shahada yake ya Mass Communication Makerere University Uganda
2. Alikuwa Ripoter wa Radio One na ITV kwa muda mrefu akitumia jina la Deo Haule akiripoti toka Kampala
3. Alijiunga na Jeshi la Polisi na kufanya kazi kwa mwaka mmoja kisha akaacha kazi sababu alipangiwa kitengo cha Habari makao makuu ya Polisi na kufanya kazi chini ya Mohamed Mhina ambaye hana hata degree moja
4. Alipotoka Polisi alijiunga na World Vision kama Communication/ Information Officer na kufanya kazi kwa miaka kama minne hivi akiwa Makao makuu Arusha na baadae akahamishiwa tawi la dar es salaam
5. Alipotoka World Vision akajiunga na MKURABITA ambapo alifanya kazi kwa muda usiozidi miaka miwili akaacha.
6. Baada ya kuacha Mkurabita, akafungua duka lake la electronics lipo Benjamin Mkapa Tower, opposite na Posta Mpya ghorofa ya kwanza. Then akaafungua vituo vyake vya kuuzia mafuta Ludewa na ndipo akaanza harakati za kuingia kwenye siasa na kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010.
0 comments:
Post a Comment