BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UNDANI WA KIFO CHA MWENYEKITI MWENZA UKAWA DK EMMANUE MAKAIDI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015 NA HATIMA YA JIMBO LA MASASI.

Na Sauli Giliard
Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD) Dk Emmanuel Makaidi amefariki jana katika hospitali ya Nyangao mkoani Lindi mchana, familia yake yathibitisha.

Akithibitisha taarifa hizo, mke wa marehemu, Modesta Makaidi amesema mwanasiasa huyo machachari amefariki dunia baada ya kupatwa na shinikizo la damu na amefia hospitali ya Nyangao alipopelekwa kupatiwa matibabu.

Akihojiwa na moja ya vituo vya redio jijini Dar es Salaam, afisa habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Ukawa, Tumaini Makene amethibitisha kutokea kwa msiba huo.

Mbali na kukiongoza chama chake hicho, Dk Makaidi alikuwa akigombea ubunge jimbo la Masasi kupitia NLD ambacho ni moja ya vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Mwanasiasa huyo machachari ndiye aliyekuwa mwenyekiti mwenza wa Ukawa na alikuwa miongoni mwa wanasiasa walioonyesha msimamo mkali katika Bunge la Katiba.


Dk Makaidi alizaliwa Aprili 10, 1941 huko wilayani Masasi mkoani Mtwara na ameshawahi kufanya kazi serikalini kabla kujitosa katika siasa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: