Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki
za Binadamu, Dk Helen Kijo-Bisimba baada ya kupata ajali na kufanyiwa upasuaji, Dar es Salaam leo.
Dar
es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),
Dk Hellen-Kijo Bisimba amepata ajali ya gari na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za
mwili wake, ajali
hiyo ilitokea jana asubuhi katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Akiwa
katika Hospitali ya Aga Khan alikolazwa majeruhi huyo, Mkurugenzi wa Fedha na
Utawala wa LHRC, Ezekiel Masanja alisema Dk Bisimba alipata ajali katika
barabara hiyo alipokuwa akitokea kanisani.
“Gari
alilopanda liligongwa sehemu ya ubavuni na kuzunguka mara nne. Dereva wake
anaendelea vizuri lakini Dk Bisimba aliwahishwa moja kwa moja katika chumba cha
dharura,” alisema Masanja.
Hata
hivyo, Masanja hakuwa tayari kubainisha zaidi sehemu zipi za mwili alizopata
majeraha Dk Bisimba, badala yake alisema wanasubiri ripoti kutoka kwa daktari
ndipo watoe taarifa.
Baadaye
mchana jana, Dk Bisimba alitolewa kwenye chumba cha dharura na kuhamishiwa
wodini kuendelea na matibabu zaidi.
Akizungumza
jana jioni, Mkurugenzi wa Utetezi wa kituo hicho, Harold Sungusia alisema kuwa
bosi wake anaendelea na matibabu na kuna dalili za kufanyiwa upasuaji wa mguu
wa kushoto.
Alisema kuwa kwa sasa wanasubiri maelekezo zaidi
kutoka kwa madaktari.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ DK MAGUFULI AIBUKIA HOSPITALI YA AGA KHAN AKIMJULIA HALI KIJOBI-SIMBA DAR ES SALAAM.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment