BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UJUE WEMA WA ASKARI WA JESHI LA POLISI TANZANIA WAKATI WA MATUKIO YA UOKOAJI.

TUKIO HILI LILITOKEA OKTOBA 12 MWAKA 2013 NA LEO MTANDA BLOG INAANGAZIA JAPO KIDOGO KAZI ZA JESHI LA POLISI TANZANIA KWA RAIA.

JESHI HILO MOJA YA MAJKUMU YAKE KUSAIDIA UOKOAJI KATIKA MAJAMBA MBALIMBALI KAMA TUKIO HILO LA RAIA WA KIGENI.

RAIA HAO WALIOKUWA WAMEPAKIWA KATIKA LORI NA KUKAA SAMBAMBA NA MIFUKO ILIYOJAZWA CHOKAA IKISAFIRISHA KUTOKA DAR ES SALAAM KUELEKEA MIKOA YA NYANDA ZA JUU KUSINI KABLA YA RAIA WEMA KULITILIA SHAKA NA KUTOA TAARIFA KWA JESHI LA POLISI.

HALI HIYO ILISAIDIA KUWAOKOA RAIA 16 WALIOKUWA WAMEZIDIWA KUTOKANA NA KUVUTA HEWA CHAFU.

Askari wa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro wakimpatia huduma ya kwanza raia wa ethiopia baada ya gari lao walikuwa wakisafiria kukamatwa eneo la Msamvu wakati wakielekea nchini Malawi ambapo waethiopia 16 walikamatwa kati yao wanne walikimbizwa hospitali ya mkoa huo baada ya kuishiwa nguvu mkoani hapa. 


Raia hao walipakiwa sambamba na mifuko ya chokaa hali iliyosababisha kuvuta hewa chafu na kupelekea kuishiwa nguvu.







Mkuu Msaidizi wa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro Seleman Mpamba kushoto akisaidia na askari wake kumpeleka raia wa ethiopia katika gari baada ya kuishiwa nguvu mara baada ya gari lao kukamatwa wakati wakielekea nchini Mawali eneo la Msamvu mkoa wa Morogoro, Lori hilo lilibeba raia hao kwa kuwapakiza sambamba na mifuko ya chokaa.

Askari kanzu na mwenye sare akimnyeshwa maji mmoja wa waethiopia hao.

Clement Bazo akigawa unga wa kurejesha nguvu mwilini kwa waethiopia hao ambao waliishiwa nguvu kutokana na kufuta hewa iliyochanganyikana na chokaa.

Mkuu Msaidizi wa kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro Seleman Mpamba akiwa amempatia msaada muethiopia baada ya kuishiwa nguvu mara wakati wakipatiwa huduma ya kwanza katika kikuu cha polisi.

Wasamalia wema wakimchomoa raia wa ethipia katika tela la lori kituo kikuu cha polisi mkoa wa Morogoro baada ya wasamalia hao kulitilia mashaka lori ambalo baadaye waligundua kuwepo kwa raia 16 kwa raia hao eneo la Msamvu Manispaa ya Morogoro



 

Hapa akitelemka kutoka kwenye lori hilo lililokuwa limepakia chokaa.PICHA KUTOKA MAKTABA YA MTANDA BLOG.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: