MAAFISA WANNE WA JESHI LA POLISI WAFUNGWA MIAKA 15 JELA KWA KUMFANYIA UKATILI DEREVA TEKSI KISHA KUFARIKI DUNIA BAADA YA KUMBURUZAN NA GARI.
Maafisa wanane wa polisi waliopatikana na hatia ya kumtendea unyama dereva wa teksi kutoka Msumbiji mwaka 2013 wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja.
Jaji Bert Bam amesema kitendo walichofanya maafisa hao wa polisi ni cha kinyama.
Baada ya kuwaagiza wasimame kizimbani, amewaambia "kila mmoja wenu anahukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.”
Jaji huyo amesema mauaji hayo hayakukusudiwa.Maafisa hao walinaswa kwenye kanda ya video wakimbrurura dereva wa teksi kutoka Msumbuji aliyetambuliwa kama Macia mwenye umri wa miaka 27 mtaa wa Macia mashariki mwa Johannesburg.
Macia alikuwa amesimamishwa na maafisa tisa wa polisi kwa kosa la kuvunja sheria za trafiki, lakini baadaye kukatokea mfarakano.
Mmoja wa maafisa hao hakupatikana na hatia.
Video ya kisa hicho ilisambaa sana katika mitandao ya kijamii.
Ukumbi wa mahakama mjini Johannesburg ulikuwa umejaa jamaa za maafisa hao wa polisi pamoja na wanahabari.
Raia waliozungumza na BBC wanasema hukumu hiyo itakuwa funzo kwa maafisa wa polisi dhidi ya kutumia vibaya mamlaka yao wakiwa kazini.
KISA CHENYE NDIYO HIKI.
Ukatili wa polisi Afrika Kusini.
28 Februari 2013.
Kamati maalumu ya kuangalia shughuli za polisi huko Afrika kusini inachunguza kisa ambacho dereva mmoja wa Taxi raia wa Msumbiji alifungwa nyuma ya gari la polisi na kuburutwa katika barabara za mji wa Johannesburg.
Dereva huyo aliripotiwa kufariki baadaye wakati alippokuwa kizuizini.
Picha ya Video iliyorekodiwa na mpita njia imekuwa ikionyeshwa katika vyombo vya habari vya kitaifa nchini Afrika kusini.
Shirika la Amnesty International limesema kuwa picha hiyo ni dhihirisho la hofu ambayo wamekuwa nao kwamba visa vya ukatili wa polisi vinazidi kuongezeka nchini Afrika kusini.
Msemaji wa polisi alisema alishtishwa na kisa hicho.
Vyombo vya habari vilisema kuwa polisi walimtendea ukatili dereva huyo baada ya kumtuhumu kwa kuegesha gari lake visivyo, mashariki mwa Johannesburg.
0 comments:
Post a Comment