BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MTOTO WA CELINA KOMBANI AWAHENYESHA CHADEMA NA ACT-WAZALENDO JIMBO LA ULANGA KATIKA UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE MOROGORO

Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Ulanga, Isabela Chilumba akimpongeza mshindi katkka kinyang'anyiro cha ubunge jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga baada ya kuibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Ulanga kufuatia kuwashinda wapinzani wake wa Chadema na ACT-Wazalendo kwa kupata kura 25,902 sawa na 69.78% katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga Novemba 23 usiku mkoani Morogoro.

Na Juma Mtanda, Mwananchi.
Chama cha mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Ulanga baada ya mgombea wake, Goodluck Mlinga kupata kura 25,902 sawa na asilimia 69.78 akiwashinda wapinzani wake katika uchaguzi uliofanyika jana wilayani Ulanga mkoa wa Morogoro.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ulanga Novemba 23 usiku. Isabela Chilumba alimtangaza mgombea wa CCM, Goodluck Mlinga kuwa ndiyo mshindi wa kiti hicho baada ya kuwabwaga wenzake wa chama chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) na ACT-Wazalendo.

Uchaguzi huo umefanyika Novemba 22 ikijumuisha vituo vya kupigia kura 203 katika kata 21 huku kukiwa na idadi ya wapigakura 76,715 waliojiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura.

Jumla ya wapigakura 37,499 walijitokeza kupiga kura huku kura 379 zikiharibika wakati kura halali zikiwa 37,120.

Vyama vitatu vya siasa ikiwemo chama cha Mapinduzi (CCM) kikiwakilishwa na Goodlack Mlinga wakati chama cha Demokrasia na Manendeleo (CHADEMA) Pancras Michael Ikongoli na chama cha ACT Wazalendo, Isaya Maputa.

“Kwa mamlaka niliyopewa na tume ya taifa ya uchaguzi, namtangaza mgombea wa CCM, Goodluck Mlinga kuwa mshindi wa kiti cha ubunge jimbo la Ulanga baada ya kupata kura 25,902 sawa na asilimia 69.78% baada ya kuwashinda wenzake wa Chadema na ACT-Wazalendo”.alisema Chilumba.

Mgombea wa CHADEMA Pancras Michael Ikongoli alipata kura 10,592 sawa na asilimia 28.53% wakati mgombea kupitia ACT-Wazalendo yeye akipata kura 6,26 sawa na asilimia 1.69%.

Kwa upande wa mgombea wa CCM, Goodluck Mlinga aliwashukuru wananchi wa jimbo la Ulanga kwa kumchagua kuwa mbunge wao na kuahidi kuitumikia kazi hiyo kwa moyo mmoja na kuomba ushirikiano kutoka kada mbalimbali ili kutekeleza majukumu yake hayo mapya.

“Nina kazi ngumu ya kutekeleza ahadi nilizo ahadi kupitia ilani ya chama changu kwa mwaka 2015/2020 ila kwa uwezo wa mwenyezi mungu nina imani nitakeleza ahadi hizo kupitia ushirikiano wa viongozi wangu wa chama, serikali na wananchi”.alisema Mlinga.

Matokeo hayo yalitangazwa jana majira ya saa 7 usiku kumkia jumatatu ya November 23 kukiwa na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi kutoka tume ya taifa ya uchaguzi kufuatia kumalizika kwa kazi ya zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi mdogo uliofanyika jimboni hapo.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Ulanga, Christina Mndeme alieleza kuwa uchaguzi huo ulifanyika kwa hali ya amani na utulivu.

Jimbo la Ulanga halikufanya uchaguzi wa nafasi ya mbunge katika uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu, kutokana na tume ya uchaguzi kuhairisha uchaguzi wa mbunge, kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa jimbo hilo Marehemu Celine Kombani.

Wakati tukio la kutangazwa matokea hayo katika ukumbi huo wa Halmashauri Ulanga, wagombea wa Chamde na ACT-Wazalendo hawakuweza kuonekana kutokana na sababu mbalimbali.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: