WANANCHI 7 WAFYATULIWA RISASI MWILINI NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO KATIKA KUMBI YA STAREHE.
Watu wenye silaha wamewapiga risasi na kuwauwa watu saba usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Burundi- Bujumbura
Watu hao waliokuwa katika kilabu cha burudani mjini Bujumbura waliamrishwa walale chini kabla ya kufyatuliwa risasi na kuuawa papo hapo.
Meya wa mji huo ametaja kisa hicho kama mauwaji ya kinyama.
Waliwauawa 7 na kuwajeruhi wengine wawili alisema Freddy Mbonimpa meya wa mji huo.Awali wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu
Mauaji hayo yanatukia katika siku ya mwisho iliyotolewa na serikali kwa raia walioko na silaha kuzisalimisha kwa vyombo vya dola.
Awali Serikali ilikuwa imewapa watu fursa ya kusalimisha silaha walizo nazo lau sivyo polisi wachukue hatua kali dhidi yao kuwapokonya.Katika juma lilopita pekee , watu 20 wamekufa, hasa kwenye mitaa ambako upinzani una nguvu.
Hapo jana wenyeji wa vitongoji vya mji wa Bujumbura walionekana wakitoroka makwao kwa hofu ya makabiliano na vyombo vya serikali.
Mwandishi wa BBC mjini Bujumbura, aliwaona watu wamebeba magodoro na kadhalika katika mabarabara, wakihamia kwenda kwa marafiki na jamaa katika mitaa salama.BBC
0 comments:
Post a Comment