Rais mpya wa Tanzania John Magufuli leo amefanya ziara ya kushtukiza katika Hazina Kuu siku moja tu
Rais huyo amefanya ziara hiyo fupi kutoka ikulu muda mfupi baada ya kumuapisha Mwanasheria Mkuu George Mcheche Masaju.
Masaju aliteuliwa mara ya kwanza kuwa Mwanasheria Mkuu na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Januari mwaka huu baada ya kujiuzulu kwa George Werema.
Magufuli hakuzungumza rasmi na wanahabari baada ya kumaliza ziara hiyo.
Hata hivyo, mwandishi wa BBC Tulanana Bohela anasema kuna uwezekano amezungumza na maafisa wa hazina kuu kuhusu hali ya mikopo ya wanafunzi.
Wakati wa kampeni, Magufuli aliahidi kufanya elimu kuwa bila malipo kuanzia shule za msingi hadi shule za sekondari.
Magufuli ameagiza Bunge lifunguliwe Novemba 17 na anatarajia kuwasilisha jina la Waziri Mkuu wake kwa bunge hilo Novemba 19.
Magufuli aapishwa kuwa rais mpya Tanzania
John Pombe Magufuli sasa ndiye rais mpya wa taifa la Tanzania baada ya kuapishwa rasmi kufuatia ushindi wake wa wingi wa kura katika uchaguzi mkuu uliopita.
Akiapishwa katika hafla iliohudhuriwa na viongozi mbalimbali,wakiwemo marais kutoka mataifa ya Afrika mashariki na kusini, Magufuli ameapa kutimiza ahadi zote alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Magufuli ambaye sasa ni rais wa awamu ya tano nchini Tanzania vilevile amewataka viongozi wa upinzani nchini humo kukubali kushindwa na kushirikiana naye katika juhudi zake za kuimarisha maisha ya taifa hilo.
Amesema kuwa licha ya kwamba alipata changomoto kubwa kutoka kwa upinzani alioupata amepata funzo kubwa kutoka kwao.
''Nashukuru wagombea wenzangu kwa kutupa changamoto,tumejifunza mengi kutoka kwao,lakini pia wajue kwamba uchaguzi umekwisha na rais ni John Pombe Magufuli'',alijigamba.
Rais aliyeondoka madarakani Jakaya Mrisho Kikwete
Amesema kuwa licha ya kwamba alipata changomoto kubwa kutoka kwa upinzani alioupata amepata funzo kubwa kutoka kwao.
''Nashukuru wagombea wenzangu kwa kutupa changamoto,tumejifunza mengi kutoka kwao,lakini pia wajue kwamba uchaguzi umekwisha na rais ni John Pombe Magufuli'',alijigamba.Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo.
Awali aliyekuwa rais wa taifa hilo Jakaya Mrisho Kikwete aliwasili katika uwanja wa sherehe hiyo mbele ya umati mkubwa wa watu waliomkaribisha kwa vifijo na nderemo.
Kikwete aliuzunguka uwanja huo akiwapungia mkono wa kwaheri raia hao waliojaa uwanja huo.
Baadaye Bendera ya utawala wake ilishushwa huku rais mpya John Magufuli akiapishwa na makamu wake wa rais Samia Suluhu Hassan.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / kitaifa /
slider
/ ZIARA YA RAIS DK MAGUFULI YA KUSTUKIZA KATIKA WIZARA YA FEDHA AWAKAMATA WAFANYAKAZI WATORO DAR ES SALAAM.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment