BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

AFUATA NYAYO: MTOTO WA CELINA KOMBANI AANZA VURUGU KATIKA UJENZI WA ZAHANATI NA KITUO CHA POLISI JIMBO LA ULANGA BAADA TU YA KUKABIDHIWA CHETI CHA UBUNGE MORO.


Mbunge Mteule wa jimbo la Ulanga, Goodluck Asaph Mlinga (32) kulia akisikiliza jambo kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Mbangayao, Devid Eponda mbele ya jengo la ofisi ya mwalimu mkuu katika kitongoji cha Isaka kufuatia majengo ya shule hiyo kuvunjwa na serikali kupisha hifadhi ya misiti ya Mbangayao hivi karibuni.

Na Juma Mtanda/MTANDA BLOG.
Wananchi wa jimbo la Ulanga wamemchagua mtoto wa kwanza wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani (56), Goodluck Mlinga (32) kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo uliofanyika Novemba 22 mwaka huu.

Mbunge huyo wa jimbo la Ulanga aliwashinda wapinzani wake katika uchaguzi mdogo wa ubunge baada ya kupata kura 25,902.69.78% huku mgombea wa Chadema, Pancras Ikongoli alikapata kura 10,592.28.53% wakati wa ACT-Wazalendo Issaya Maputa akipata kura 626.169%.
Mbunge Mteule jimbo la Ulanga, Goodluck Mlinga kushoto akizungumza jambo na Ibrahim Mkingi (22) mmoja wa wahanga waliochomewa nyumba sita moto, zinazomilikiwa na wanaCCM ambazo zilichomwa moto usiku wa saa 8 Novemba 24 mwaka huu katika kijiji cha Iputi kata ya Mbunga tarafa ya Mwaya wilaya ya Ulanga. 

Goodluck Mlinga ndiye mtoto wa kwanza wa Celina Kombani kati ya watoto watano, lakini kijana huyo tayari ameonyesha moyo wa dhati wa kuwatumikia wananchi kwa kutatua kero na baadhi ya changamoto mbalimbali kupitia ngazi hiyo ya ubunge.

Goodluck Asaph Mlinga (32) amefunga ndoa na mkewa Emma Mhezi miaka michache iliyopita na kupata watoto wawili, Glory Goodluck Mlinga (5) na Mathew Goodluck Mlinga huku akiwa na wadogo zake Godfrey Mlinga, Lucy Damas, Joely Damas na Shaban.
Mlinga ameonyesha moyo huyo kwa kuanza na kazi ya uanzishwaji wa ujenzi wa jengo la zahanati kijiji cha Mbangayao kilichopo kitongoji cha Isaka sambamba na ujenzi wa kituo cha polisi kijiji cha Iputi na ukarabati wa nyumba sita za wanaCCM ambazo zilichomwa moto Novemba 24 mwaka huu kwa itikadi za kisiasa.
Mbunge jimbo la Ulanga. GOODLUCK ASAPH MLINGA (32).

Sambamba na majukumu hayo tayari zimeanza kutumika kiasi cha fedha Sh3 Milioni, ikiwemo katika kijiji cha Mbangayao kilichopata sh1 Milioni za zahanati huku Iputi ikipata sh2 Milioni kwa ajili ya kituo cha polisi na ukarabati wa nyumba sita zilizochomwa moto.

Kufanya kazi hizo, hakukufanya aweze kusubiri kuapishwa bungeni Dodoma bali ilimlazimu kusubiri kupata cheti cha kumdhibitisha kuwa mbunge wa jimbo hilo la Ulanga ili kufanya kazi za kuwatumikia wananchi baada ya kushinda uchaguzi huo.

Akizungumza na MTANDA BLOG katika mahojiano maalum mjini Mahenge mkoani Morogoro, Goodluck Asaph Mlinga (32) alieleza kuwa kazi ya kuwatumikia wananchi haitampa wasiwasi wowote kutokana na kujifunza mambo mengi kupitia kwa mama yake wakati wa uongozi wake kabla ya kufariki dunia.

“Nimejifunza mambo mengi ya uongozi kutoka kwa mama yangu mpendwa Celina Ompeshini Kombani akiwa mbunge hadi vyeo mbalimbali alivyokuwa akiwatumikia watanzania ndani ya serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) (mwenyezi mungu ampe mwanga wa milele amwangazie apumzike kwa amani…amina).”alisema Mlinga.

Goodluck Asaph alizaliwa Februar 27 mwaka 1982 Morogoro mjini na kupata elimu ya msingi katika shule ya Ukwama mwaka 1990-1996 Mahenge huku akijiunga na kidato cha kwanza mwaka 1997 hadi 2000 katika shule ya sekondari Pugu Dar es Salaam wakati kidato cha tano na sita akihitimu elimu hiyo katika sekondari ya Kigurunyemba mwaka 2002 hadi 2004 mjini Morogoro.

Mlinga pia amehitimu elimu ya chuo kikuu cha Mzumbe kilichopo wilayani Mvomero kwa shahada ya utawala mwaka 2005 hadi 2008 wakati astashahada ya sheria ya upatanishi na ushuluhisho ya chuo cha ustawi wa jamii kwa mwaka 2010 hadi 2012 jijini Dar es Salaam.

“Baada ya kupata elimu hiyo nilianza kazi kama afisa Tawala wizara ya Maendeleo ya jamii kwa mwaka 2012-2013 na mwaka 2013 hadi mwaka 2015 nilifanya kazi mfuko wa bima ya taifa ya afya kama Afisa Matekelezo.”alisema Mlinga.

Mlinga alijinasibu kwa kusema kuwa ili kuweza kumuenzi vyema mama yake Celina Kombani ni kuendeleza mipango yake ya maendeleo kwa wana Ulanga na Tanzania kiujumla.

“Mama alikuwa na mipango mingi ya maendeleo katika jimbo hili la Ulanga, moja ya mipango hiyo kujenga chuo kipya cha Ufundi Stadi (VETA) ili kiweze kutoa elimu ya ufundi kwa wanafunzi waliokosa kuendelea na elimu kwa ngazi mbalimbali kuanzia wale wa darasa la saba, kidato cha nne na kuendeleo.”alisema Mlinga.

Aliongeza kuwa ili kuendelea mpango huo tayari kimetengwa kiwanja maalumu kijiji cha Mwaya na kazi iliyopo mbele yake ni kufuatilia utaratibu kwa viongozi wa VETA Kanda ya Mashariki kuona Mama aliishia wapi na kuendelea na hatua iliyobakia.
Mbunge wa jimbo la Ulanga, Goodluck Asaph Mlinga (32) (aliyekaa kwenye kiti) akizungumza na akinamama wa kitongoji cha Kipingu baada ya kupatwa na msiba, tarafa ya Vigoi wilaya ya Ulanga. 

Mlinga alisema kuwa mipanga kama itaenda vizuri ndani ya miaka mitano chuo hicho kiwe kimeanza kutoa matunda na hilo linawezekana hasa kwa kushirikisha nguvu kazi ya ujenzi kwa kushirikiana na wananchi.

Mipango mingine ni kuboresha sekta ya elimu kwa walimu kuanzishiwa miradi ya shule, kuanzisha benki za kijamii vijijini (VIKOBA) na Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) na kujenga nyumba za walimu kwani mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuna upungufu wa nyumba za walimu 400.

“Nina imani nitafanikiwa kutekeleza ujenzi wa nyumba za walimu, madarasa, vituo vya zahanati, vituo vya polisi kwa kutafuta fedha kwa wafadhili lakini kutumia nguvu kazi kutoka kwa wananchi hasa katika ufyatuaji wa matofali na kutumia asilimali za mazao ya misitu kwa kufuata utaratibu.”alisema Mlinga.

Kwa upande wa afya ameweka lengo la kupanua vituo vya afya na hospitali kutumia mfumo huo huo wa kushirikisha wananchi na fedha za wafadhili na kupata magari matatu ya wagonjwa kwa ajili ya tarafa tatu za Mwaya, Lupilo na hospitali ya wilaya.

“Gari moja la wagonjwa tayari limepatikana na lipo njiani linaletwa Mahenge muda wowote na gari hili lilinunuliwa na Mama yangu na gari lingine ni ahadi ya balozi wa Tanzania nchini Kenya na lililobakia natafuta mwenyewe ili kukamilisha idadi ya magari matatu ya wagonjwa.”alisema Mlinga.

Nitaanzisha utaratibu wa Wazee kutibiwa bure kupitia mfuko wa taifa wa bima ya afya kwa kuwatafutia wafadhili na fedha za mfuko wa jimbo.aliongeza Mlinga.

“Ninachaomba kwa wananchi, serikali za vijiji, vyama vyote vya siasa na viongozi wa dini zote waniunge mkono katika jitihada za kuieletea maendeleo ya wananchi hasa katika kazi zinazohitaji nguvu kazi.”alisema Mlinga.CHANZO:MTANDA BLOG
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: