BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CHANZO CHA AJALI YA BASI LA NEW FORCR ILIYOSABABISHA ABIRIA 12 KUFARIKI DUNIA NA WENGINE 28 KUJERUHIWA NDIO HIKI MKOANI IRINGA.

Basi la kampuni ya New Force baada ya kugongana
Iringa. Abiria 12 wamefariki  huku wengine 28 wamejeruhiwa mara baada ya basi la kampuni ya New Force kugongana na lori maeneo ya Igeme, Kilolo
jana mchana.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, basi la New Force lilikuwa linatokea jijini Dar es Salaam kuelekea Tunduma, mkoani Mbeya, na baada ya kugongana na gari hilo la mizigo, yalipinduka.

Jeshi la Polisi mkoani Iringa limethibisha kutokea ajali hiyo na kuongeza kuwa majeruhi wamewahishwa hospitali ya wilaya ya Kilolo huku wengine waliokuwa taabani wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Iringa.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Iringa, madereva wa basi na lori ni miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika ajali hiyo na uchunguzi unaendelea.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: