BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAZI IMEANZA KWA SPEED !!! NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO AVAMIA KITUO CHA TIBA MBADALA LA FORE PLAN CLIN ILALA BUNGONI DAR ES SALAAM.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala jioni ya 14 Disemba 2015 amefanya ziara ya ghafla kituo cha Tiba Mbadala cha Fore plan Clinic kinachomilikiwa na Dk. Mwaka Juma Mwaka kilichopo Ilala Bungoni na kujionea hali halisi ya kituo hicho. 

Mh. Naibu Waziri pamoja na mambo mengine alifanya ukaguzi kuanzia Mapokezi mpaka vyumba vya matabibu ambapo vyote hakukuwa na Madaktari waliokuwa wanatoa huduma.


Baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakisubiri tiba walisema kituo hicho hakina uwezo wa kuhudumia wagonjwa kama inavyonadiwa sehemu mbalimbali. Naibu Waziri aliwataka wagonjwa hao waende kwenye hospitali ili wapate matibabu yanayoendana na magonjwa yanayowasumbua.


Msaidizi wa Dk. Mwaka, Bi Teddy L. Mbuya alikana kusema kuhusu kituo hicho maana yeye sio msemaji Mkuu bali alimwomba Naibu waziri kufanya ukaguzi katika kituo hicho.
Baada ya ukaguzi Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis Kigwangala alimwagiza Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asilia na mbadala Dk.Paul Mhame ndani ya wiki moja kufanya ukaguzi kwa kituo cha Dk. Mwaka na aletewe taarifa iliyokamilika kuhusu taaluma yake pamoja na washirika wake ikiwa ni pamoja na dawa anazotumia kama ni rafiki kwa watumiaji. 

 
Hiyo ni pamoja na kufanya ukaguzi wa vituo vyote vinavyotoa tiba Mbadala na Tiba asili kama Dk. Ndodi, Dk. Rahabu n.k ili kuwabaini wanaowalaghai wananchi.

Pia Mh. Naibu Waziri amepiga marufuku Matabibu wa Tiba Mbadala kujitangaza kupitia vyombo mbalimbali vya Habari hapa nchini kwa kuwa kufanya hivyo ni kosa la kimaadili ya kazi za Tiba/Tabibu. 


Alisisitiza kwa kusema Madaktari wana miiko yao na katika miiko hiyo mojawapo ni kutojitangaza.
Naibu waziri aliendelea kukemea matabibu Kama Bw. Mwaka kujiita Dokta na kuuchambua mwili wa Binadamu kama vile aliyesomea Udaktari. Aliongeza, sheria ya tiba asili na tiba Mbadala hairuhusu watu wa Tiba asilia na Tiba Mbadala kutumia maneno ya tiba ya kisasa.


Naibu Waziri alimalizia kwa kumtaka Bw. Mwaka Juma Mwaka kufika Ofisini kwake Wizarani 15/12/2015 saa mbili asubuhi akiwa na nyaraka zake zote zinazohusu utoaji wa huduma ya Tiba Mbadala kwani amekuwa akijiita majina ya tiba za kisasa na pia kutibu kwa njia ya kisasa badala ya kutibu kwa njia ya Asilia au Tabibu.CHANZO:https://www.facebook.com/nassoroally.matuzya
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: