KIMENUKA TENA !! RAIS MAGUFLI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU DK HOSEH HUKU WATUMISHI WANNE WAANDAMIZI TAASISI HIYO WAKISIMAMISHWA KAZI KWA KUSAFIRI NJE YA NCHI LICHA YA KUNYIMWA KIBALI NA RAIS.
Rais Dk John Magufuli (Kushoto) na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah (Kulia).
Dar es salaam. Rais Dk. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah kutokana na kutorishwa na namna taasisi hiyo ilivyokua ikitekeleza wajibu wake katika kukabiliana na rushwa hususani kwenye upotevu wa mapato ya serikali katika bandari ya Dar es salaam.
Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa kufuatia kutenguliwa kwa uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru.
Balozi Sefue amebainisha kuwa, Rais Magufuli amechukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kuwa utendaji kazi wa Takukuru chini ya Dk. Edward Hoseah hauwezi kuendana na kasi anayoitaka.
"Eneo mojawapo la upotevu mkubwa wa mapato ya serikali ni Bandarini na Katika Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA, Hivyo Mheshimiwa Rais amesikitishwa na kitendo cha taarifa za kuwepo kwa vitendo vya rushwa katika eneo hilo kwa muda mrefu lakini kasi ya Takukuru kuchukua hatua haiendani na kasi anayoitaka" imesisitiza taarifa ya Balozi Sefue.
Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema kuwa, Rais Magufuli ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi waandamizi wanne wa Takukuru ambao walisafiri nje ya nchi licha ya Rais Magufuli kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma.
‘’Watumishi hao ni Mary Mosha, Ekwabi Mujungu, Doreen Kapwani na Rukia Nikitas ambao walisafiri nje ya nchi licha ya kunyimwa kibali cha safari kutoka kwa Rais ama Katibu Mkuu Kiongozi’’. Imesema taarifa ya Balozi Sefue
Balozi Sefue amewataka watumishi wengine wa umma kutii agizo la Rais Magufuli na kuonya kuwa atakayekiuka atachukuliwa hatua kali.MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment