BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAHAKAMA KUU YAWAMINYA MBAVU WANACHAMA WA CUF NA KESI YAO YA KUPINGA UBUNGE JIMBO LA TABORA MJINI.


Tabora. Mahakama Kuu Kanda ya Tabora imetoa sharti kwa wanachama wanne wa Chama cha CUF kulipa dhamana ya SH9 milioni ili kesi waliyofungua kupinga matokea ya uchaguzi katika Jimbo la Tabora Mjini ianze kusikilizwa.

Sharti hilo lilitolewa jana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Amir Mruma baada ya kusikiliza maombi ya wanachama hao wanaotetewa na Wakili, Hashim Mziray.

Katika kesi hiyo namba 49/2015 ya kuomba kupunguziwa gharama ya dhamana ya kupinga matokeo ya uchaguzi, Mahakama imeamuru kila mlalamikiwa alipiwe dhamana ya Sh3 milioni.

Jaji Mruma alisema katika kesi za uchaguzi, Sheria inaitaka Mahakama iangalie kiwango cha fedha anachotakiwa mlalamikaji kukilipa kama dhamana bila kujali uwezo wake.

Aliongeza kuwa, Bunge lilitunga sheria ya gharama za kesi za uchaguzi kwa lengo la kupunguza kufunguliwa kwa mashauri mengi yasiyo na msingi.

Katika uamuzi wake, Jaji Mruma alisema amepitia maelezo ya pande zote na kuridhika na wajibu maombi kuwa walalamikaji wana uwezo mkubwa, hivyo wanapaswa kulipa Sh15 milioni ili kesi ya msingi iweze kusikilizwa.

Akifafanua, Jaji Mruma alisema walalamikaji wameshindwa kuwasilisha uthibitisho wa maombi yaliyoainishwa katika hati za viapo vyao kuwa wao ni maskini hawataweza kumudu kulipa kiwango hicho.

Awali, upande wa wajibu maombi wakiwakilishwa na mawakili Kamaliza Kayaga na Juma Masanja, waliiambia mahakama kuwa waombaji wote wanne wanapaswa kupeleka uthibitisho wa kuwa na wategemezi wengi wanaoishi nao.

Wakili Mziray alieleza kuridhika na uamuzi uliotolewa na kwamba, wateja wake watajipanga ndani ya siku 14 kulipa kiwango kilichoamriwa na Mahakama ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

Wanachama hao, Jumanne Mtunda, Johari Kasanga, Shaaban Mussa na Thomas Ayengo, walifungua kesi hiyo ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mgombea wa CCM, Emmanuel Mwakasaka.

Katika shauri hilo namba 3/2015, wanadai uchaguzi huo haukuwa huru na haki, hivyo wanaiomba Mahakama itengue matokeo yake na kumpa ushindi aliyekuwa mgombea wa CUF, Peter Mkufya.MWANANCHI
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: