BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA NIGERIA MUHAMMADU BUHARI ASHAURIWA KUFUATA NYAYO ZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.

Joto la utendaji kazi wa Rais Dk. John Magufuli, limeendelea kuwakuna wengi baada ya mwandishi wa habari nchini Nigeria, Alkasim Abdulkadir, kumshauri Rais wake Muhammadu Buhari, kuchukua walau mambo machache toka kwa Rais Magufuli ili ayatumie kuiongoza nchi hiyo.

Mwandishi huyo wa NAIJ.com amesema, wananchi wengi wa Nigeria, kama ilivyo kwa wengine barani Afrika, wamevutiwa na hatua za Dk. Magufuli hususan za kukata matumizi ya fedha za umma yasiyo ya lazima.

Mhariri mmoja nchini humo, Abang Mercy, alisema kupitia kwenye Twitter hivi karibuni:

“Toka achaguliwe, Rais Magufuli wa Tanzania amekuwa akitekeleza mabadiliko makubwa; sawa na ambao nilitegemea Rais Buhari ayafanye.”

Kwa mujibu wa Abdulkadir, maoni hayo ya Mercy ndiyo yaliyokuwa ya wafuasi wengi wa Rais Buhari ambayo walitarajia yangeonekana katika utawala wake.
Hata hivyo, Abdulkadir alisema staili ya uongozi unaoendeshwa na Dk.

Magufuli, siyo mpya katika historia ya Tanzania, kwani ndiyo uliokuwapo wakati wa uongozi wa hayati Mwalimu Julius Nyerere. Alisema miaka 30 baada ya utawala wa Mwalimu Nyerere, Tanzania imepata kiongozi wa aina hiyo ambaye alikuwa na umri wa mwaka mmoja, wakati Nyerere alipoanza kutawala na alikuwa kijana aliyekomaa wakati Nyerere alipong’atuka.

Abdulkadir alisema tangu aapishwe Novemba 5, mwaka huu, Dk. Magufuli amechukua hatua ambazo zimemfanya avute wengi barani Afrika, ikiwa ni pamoja na kukata matumizi ya kawaida kwenye shughuli za kitaifa na aina ya maisha yake. CHANZO: NIPASHE
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: